Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Video: Mwandishi wa habari ITV Arusha akamatwa na polisi kwa agizo la Mkuu wa WilayaMwandishi wa habari wa ITV mkoani Arusha Bw Khalifa Lihundi anashikiliwa na polisi kituo cha Usa River wilayani Arumeru mkoani Arusha kwa tuhuma za kuandika habari za zinazodaiwa kuwa ni za uchochezi.

Bw Lihundi amekamatwa jijini Arusha majira ya saa nane mchana na askari anayedaiwa kutumwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Bw Alexsander Mnyeti kama alivyoeleza Bw Basili Elias ambaye alishuhudia tukio hilo.

Akizungumzia suala hilo mpiga picha wa Bw Khalifand Lihundi Bw Deogratius Kassamia amesema habari inayodaiwa kuwa ni ya uchochezi ilikuwa ni ya malalamiko ya wananchi juu ya tatizo la maji.

Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Arusha Bw Cloud Gwandu pamoja na kulaani kitendo hicho amesema hatua hiyo haikubaliki kwani haikufuata taratibu.

Taarifa zaidi zimeeleza kuwa huenda Bw Lihundi akafikishwa mahakamani hapo kesho.

SOURCE: ITV HABARI
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO