Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Nassari Aisifu Serikali ya Magufuli Kwa Jitihada za Kuwaletea Maendeleo Watu wa Jimbo Lake!

Mbunge wa Jimbola Arumeru Mashariki (CHADEMA) Mh Joshua Nassari (kulia) akifurahia jambo wakati wa mkutano wa majumuisho ya ziara ya Waziri Mkuu Mkoani Arusha leo. Kulia kwake ni Mbunge wa Monduli pia kupitia CHADEMA Mh Julius Kalanga.

Arusha
Mbunge wa Arumeru Mashariki kupitia CHADEMA, Mh Joshua Nassari amesifu jitihada zinaazochukuliwa na Serikali ya Rais John Pombe Magufuli kuhakikisha wananchi hasa wa Jimbo lake wanapata maendeleo.

Nassari ameyasema hayo katika kikaoha majumuisho ya ziara ya siku 10 Waziri Mkuu mkoani Arusha iliohitimishwa jana na kusisitiza kuwa kitendochaWaziri Mkuu Kassim Majaliwa kuweka mikakati ya kushughulikia migogoro ya ardhi iliyodumukwa miaka mingi ni ushahidi kwamba Serikali imedhamiria kusaidia wananchi wa kawaida. 

"Kama kuna kiongozi ambaye hawezi kuunga mkono jitihada zinazochukuliwa na viongozi hasa wa juu wa Serikali za kuwaletea maendeleo.labda huyo ni mwendawazimu. Mwaka 1952 wazee wa Meru walituma mtu kwenda Uingereza kwenda kuombauhuru wa wananchi wa Arumeru kujitawala katika kumiliki ardhi yao kutoka kwa wakoloni waliokuwawakiwanyanyasa, lakini miaka 55 baada ya Uhuru, bado migogoro na mateso hayo yapo" alisema Nassari. 

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO