Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Olesendeka na wateule wengine waapishwa rasmi leo Ikulu Dares Salaam kutumikia nafasi mpya

Rais Magufuli hii leo amewaapisha viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa mpya wa Njombe Mh Christopher Olonyike Ol-Sendeka anayechukua nafasi ya Dkt rehema Nchimbi ambaye amahamishiwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Wengine walioapishwa na Rais Magufuli hii leo ni Mhadisi MathewMtigume ambaye anakuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo (Kilimo), Dkt Maria Sasabo Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Dkt Aloyce K. Nzuki kuwa Naibu Kaibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii na Bibi Grace Alfred Martin kuwa Balozi (Mkuu wa Itifaki)

Wateule wa Rais wakila kiapo cha utii na uaminifu

Picha ya pamoja mara baada ya kula kiapo

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO