Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TAARIFA YA MEYA WA JIJI LA DAR KUHUSIANANAUTARATIBU MPYA WA KUEGESHA GARI NA PIKIPIKI MIJINI

Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akifafanua jambo kwa wandishi wa habari leo kuhusiana na suala zima la tozo za maegesho ya magari na pikipiki

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Ndugu wanahabari, 

Nimewaita leo ili kuweza kutoa ufafanuzi wa kero zinazoendelea hapa jijini Dar es salaam kuhusiana na suala zima la Paking.  imekuwa ni muda sasa zaidi ya wiki 2 na hatujatoa ufafanuzi nimeona ni busara niwajuze Wananchi wa jiji hili kujua kwamba nikitugani hivi sasa kinachoendelea.

Ndugu wanahabari,
Kumekuwa na tabia za wakandarasi wetu au kwa kutokujua au wanajua kwamba kitu gani ambacho wanapaswa kukisimamia katika jiji hili kama ambavyo mkataba unavyo elekeza. Lakini kuna hali ambayo imejitokeza ambayo sio nzuri kwa wafanya kazi wao,  wamekuwa wakiwaonea wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwa kuwakamata  hovyo hovyo na eti wanatimiza sheria ndogo ya jiji [Kanuni].

Ukiangalia majukumu ya kimkataba ambayo jiji tuliwapa ,na kukubaliana nayo ni kama ifuatavyo.

 1 .Wakala atafanya kazi hii bila Kuvizia magari ya wananchi kwa lengo la kujipatia pesa .

2. Wakala atafanya kazi hii kwa weledi mkubwa kwa kuzingatia Sheria, Miongozi, Maelekezo, Kanuni na taratibu zilizopangiwa pasipo kusababisha bughuza ,kero na usumbufu kwa Wananchi.

3. Wakala anatakiwa kutoa muda wa dakika sitini [60] kabla ya kuchukua mamuzi ya vuta gari, Bodaboda  au bajaji lilovunja sheria, kuzuia . Lakini kwa gari , Bajaji au Bodaboda iliyozuia barabara itaondolewa mara moja ili kuondoa msongamano.

4.Wakala anapaswa kuepuka kutoa Lugha ya Matusi au udhalilishaji .

4.Wakala anapaswa  kuruhusu gari ,Pikipiki au Bajaji kuegeshwa kwa dharura sehemu isiyoruhusiwa kwa muda usiozidi dakika Thelasini [30] kama Dereva ameweka viashiria vya tahadhari. Isipokuwa kwa wale wenye magari yenye hitilafu inaweza kuzidi mpaka saa moja [yaani dakika 60] baada ya kujirizisha na dharura iliyojitokeza.

5. Wafanyakazi wanapaswa kuwa na sare pamoja na vitambulisho vya kazi .

6. Wakala anatakiwa  kutoa faini zilizoainishwa na jiji na sio vinginevyo.

7. Wakala anapaswa kutumia risiti za mashine za Kielekronikia.

8.Magari yanayotumika katika utekelezaji wa kazi hii yanatakiwa yawe na Stika kubwa inayoonyesha jina la kampuni pamoja na namba ya simu ya wakala.

9.Wakala anatakiwa kutumia risiti [Point of Sale, [POS] za Halmashauri ya jiji.


10. Wakala anatatakiwa kutoa taarifa ya utekelezaji wa kazi hii kwa MWAJIRI Kila baada ya Wiki Mbili.

11.Wakala anatakiwa kufanya kazi katika maeneo aliyoelekezwa na MWAJIRI nasio vinginevyo.

12. Wakala anapaswa kushirikiana na jeshi la polisi pamoja na Mamlaka zingine pale inapohitajika katika utekelezaji wa kazi husika.

Ndugu wanahabari,
Kwa halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, kampuni ambayo ina mkataba na jiji ni Priscanne Enterprises LTD, nasio kampuni nyingine ambazo zimejitokeza.hii ndio kampuni ambayo imepewa tenda ya kufanya kazi hiyo.

Baada ya kutoa ufafanuzi huu sasa natoa maagizo yafuatayo.
Mawakala wanatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na kanuni za mikataba ambayo imelekeza nasio kufanya kazi kama wanavyotaka wao. 
Ni marufuku wakala kutumia lugha chafu na hivyo wanatakiwa wafanye kazi kwa kuzingatia majukumu ambayo wamepewa na jiji. Mambo ambayo ninayaona wanafanya kwa wananchi wa Dar es Salaam sijapendezwa nayo , naninawataka waache mara moja tabia hizo.
Ndugu wanahabari ,
Napenda kuwaagiza wakandarasi wote kwamba kuanzia Januari 2, 2017 ni marufuku kwa mtu yoyote kulipa pesa na kupewa stakabadhi ya mkono. Nawataka wakandarasi waliopewa jukumu la kukamata magari yaliyoegeshwa kwenye sehemu zisizo ruhusiwa [Wrong Parking] na kuwatoza faini kwa kosa hilo na wale wanatoza sehemu halali kuhakikisha wanatumia mashine zetu za Jiji [POS). Hii inatokana na kwamba tumegundua tunapoteza mapato mengi sana kwa sababu ya kutotumia [POS].

Ndugu wanahabari
Mwiso, ninawatakia Wakazi wote wa Jiji la Dar es Salaam  Kheri ya  Sikukuu ya Krismas na Mwaka mpya {2017} wenye mafanikio.
Ninawaomba Wazazi wote kuwa makini na watoto wao katika kipindi chote cha sikukuu zilizopo mwishoni mwa mwaka ili waweze kuvuka salama na kuanza mwaka mpya wakiwa na furaha.
Pia ninawataka Wazazi wote watakaotembelea maeneo mbalimbali na familia zao  kama vile Kando kando ya fukwe zetu za Bahari kuwa karibu na watoto wao ili waweze kuhakikisha wanajiepusha na kupotea kwa watoto na ajali mbalimbali ikiwemo za barabarani na zile za ufukweni. 
Pamoja tujenge Jiji letu.
Imetolewa na Isaya Mwita
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam.

Leo Desemba 21 mwaka 2017
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO