Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MillardAyo Video: Taarifa ya Jeshi la Polisi kuhusu miili 7 iliyopatikana Mto Ruvu na kupotea kwa Ben Saanane

Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishna Robert Boaz. Picha na MillardAyo.ComJana Disemba 21, 2016 Jeshi la Polisi Makao Makuu limetoa taarifa kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishna Robert Boaz juu ya kupatikana kwa miili ya watu 6 eneo la mto Ruvu pamoja na kupotea kwa Ben Saanane ambaye ni msaidizi wa mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe.

Katika taarifa yake, Kamishna Boaz amesema polisi walipokea taarifa za kupotea kwa Ben Saanane mnamo December 5 2016 na tayari jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kubaini mahali alipo kiongozi huyo kutoka chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema.

Aidha jeshi hilo limetoa ufafanuzi kuhusu kupatikana kwa miili sita ya watu iliyookotwa ikiwa kwenye maguni pembezoni mwa mto Ruvu, Jeshi la polisi limesema kuwa bado wanaendelea na uchunguzi ili kufahamu watu hao ni akina nani ni sababu zipi zilizopelekea kifo chao.
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO