Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

BAVICHA watoa siku tatu wapate majibu ya alipo Ben Saanane



Baraza la Vijana Taifa Tumesikitishwa sana na mwenendo usioridhisha katika ufuatiliaji hafifu wa kutoweka wa Raia wake maarufu BEN SAANANE aliepotea katika Mazingira Tatanishi yanayohatarisha haki yake ya Kuishi.

Uzito na nguvu za kipelelezi kwa amri ya Mhe. Waziri Mkuu Kumtafuta mnyama Maarufu FARU JOHN katika mbuga za wanyama unazidi mapenzi ya Serikali kwa Raia wake? Kama sivyo basi amri na uzito huo tuuone sasa kwa kumsaka BEN APATIKANE awe hai au mfu (“Dead or Alive”) nahatua za kisheria zichukuliwe kwa watenda kadri ya Taarifa za Uchunguzi.

Tulikaa kimya ili kupisha hekima na busara za viongozi wetu katika chama na Serikali pia wasimamizi wa sheria ili wajiongoze katika kuitafuta haki, kuilinda haki na kutetea haki ya uhai na uhuru wa binadamu zilizo mashakani kinyume na sheria ya nchi.

Tulitegemea kuwa viongozi wetu wanajua kuwa kuchelewesha haki ni sawa na kuinyima haki au kutotenda haki. Jambo hili tunalifananisha na Matukio ya kinyama rejea Kesi ya John D. Auko Comm. No. 232/99(2000) Aliefukuzwa kenya kwa sababu ya kutoa msimamo wa maoni yake kisiasa.

kabla ya kuondoka alitekwa nyara na kuwekwa kizuizini bila kufikishwa mahakamani kwa miezi kumi katika “notorious basement cell of Secret Service Department HeadQuorters- Nairobi na kwakufanya hivyo nchi yua Kenya ilikua imekiuka Ibara ya 5,6,9,10 na 12 ya Mkataba wa Afrika wa haki za Binadamu na Watu- 1981/1982. Tukumbuke Tanzania pia ni nchi mshirika na Ibara tajwa hapo juu za Mkataba wa Afrika katiba zimo pia katika katiba ya JMWT.

Katiba yetu ya mwaka 1977 inatoa haki ambazo kila kiongozi ameapa kuzilinda, kuzitetea na kuzitekeleza :-
Haki ya kuishi Ibara ya 14, Serikali wanawajibu namba moja wa kulinda Raia wake na mali zao, pili ni jamii na tatu ni vyombo vya kikanda na kimataifa.

Ibara ya 28 kazi ya ulinzi wa taifa, watu na mali zake ni yetu sote na zimekasimiwa Mhe. Rais kama mlinzi na mtetezi namba moja wa haki za Raia.

Mwl. J.K. Nyerere 1987 alipata kusema “ Mara nyingi Rais hutakiwa aamue hata juu ya uhai wa watu; maana hata watu wakosefu waliohukumiwa kufa kwa mujibu wa sheria hawawezi kunyongwa bila kibari rasmi cha Rais.”

HAKI YA KUISHI IKO MASHAKANI.

Ben Saanana alipo Tanzania hii, Ndugu zake hawajui, Baraza La Vijana Taifa hatujui, Chama hakijui na kila aliepaswa kujua hajui Katika hali hii sheria inaelekeza kutoa taarifa polisi baada ya hapo wajibu mkubwa na wa kwanza unahamia Serikalini kupitia vyombo vya dola vya ulinzi na usalama wanchi na Raia, kuchunguza na kumtafuta raia wake akiwa hai au amekufa kama Mtanzania bila ya kubaguliwa kwa mitazamo yake ya kisiasa.

UBAGUZI WA KIMAMLAKA.
Jambo hili ni zito na linaleta hofu kwa kila Raia wa Tanzania Je! tuko salama ikiwa mtu aweza toweka na bado mamlaka husika zenye wajibu wa ulinzi na usalama zisitoe kauli nzito na kuona jitihada za makusudi zikifanyika inai bua hisia ya uwepo wa ubaguzi.

Kwa mujibu wa ibara ya 13(4) inatoa marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au na mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya mamlaka ya Nchi. Baraza hatujaridhishwa na kasi ya ufuatiliaji wa jambo hili kwani linaibua hisia hasi kila kukicha.

Swali la msingi kujiuliza Je,
ni kwanini matukio mazito kama ubambikiwaji kesi, kutekwa nyara, uvamizi, kunyimwa dhamana, mauaji, na kubaguliwa katika huduma huwalenga zaidi wanasiasa hasa wavyama vya Upinzani na ufuatiliaji huwa hafifu? Mfano.

Mashambulio kwa wanaCHADEMA, Mauaji ya Bomu Arusha, Morogoro, Tarime, Iringa D.Mwangosi, Geita – A.Mawazo, Kupindisha sheria ama Amri za kiutawala kuwa juu ya utawala wa sheria na uhuru wa Mahakama si afya katika Amani ya Taifa letu na Serikali ya awamu ya Tano isiruhusu haya kujitikeza ama kuendelea .

UBAGUZI KATIKA KULINDWA NA KUPATA HAKI ZA KISHERIA.
Ibara ya 13(1) inavunjwa ikiwa mamlaka za kiserikali zitaendelea kukaa kimya kwani ni haki kuwa watu wote ni sawa mbele ya sheria na wanayo haki bila ya ubaguzi wowowte kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria hivyo Ben Saanane pia ni mtu kati ya hao watu wanaotajwa na katiba hivyo mdololo uliopo ikiwa utaendelea bila jitihada za ziada ni dhahiri kuwa utakua ni ubaguzi wa wazi na kunyima haki.

Mwanasiasa akitafutwa na Polisi kukamatwa, nguvu kubwa na mabavu hutumika na askari huwa wengi pia magari, heilcopter na intelligensia ya hali ya juu huwepo kulikoni hili la Ben Saanane?
Ikiwa hata dola inakuwa ngumu kwenu.

Je Nchi na raia wake wako salama? Au na sisi tungoje kupotea ama kunakosadikiwa ni kutekwa?

Hofu kwa Wananchi imetanda, hatuko salama maisha yetu na uhuru wetu watanzania uko mashakani ikiwa ukimya usio na matumaini utaendelea.

Taarifa mbalimbali za watu kuokotwa wamekufa bila kujua chanzo cha kifo, kutupwa au kuzikwa bila kuheshimu utu (human diginity) kinyume na ibara ya 12(1) inayosema “kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake”.Je kwa hivi vifo visivyotambulika kwa Maiti wanaokotwa kila mara na hata kama si raia au ni raia utu wao baada ya kifo unaondoka? Mataifa watokayo au ndugu zao watatuelewa tunapo wazika kinyama?

Ikiwa Ben Saanane anakosa au kakamatwa kwa mujibu wa mtoa onyo asiejulikana katika mtandao wa facebook rejea Ujumbe uliosomwa na Mhe. Tundu Lisu na kukabidhiwa police basi tuambiwe tujue ni kosa gani katenda, kafungwa wapi na ni kwanini hafikishwi mahakamani wala kupewa dhamana, haki ya kusikilizwa na kuwakilishwa? Taarifa za mipaka ya nchi (exit points), na viwanja vya ndege pia mitandao ya simu na mifumo mingine itumike vizuri na haraka ili kunusuru maisha yake huko aliko.

Mbali na Mhe. Waziri wa mambo ya ndani kulizungumzia katika mitandao ya jamii pia jeshi la Polisi kulizungumzia kama jambo la kawaida Vijana watanzania hatujaridhishwa na mdororo wa ufatiliaji.

PILI:

TUNAIOMBA SERIKALI ILIANGALIE SUALA LA MHE. GODBLESS LEMA KWA BUSARA NA HEKIMA YA ZIADA ZAIDI KISHERIA.

Vijana wa chadema heshima zote na bila kuathiri wala bila kuingilia uhuru wa Mahakama na kuzungumuzia shauri lililopo mahakamani. Mahakama pekee ndio itaamua itaamua kama ana hatia ua hana hatia. Isipokuwa tumeshindwa na ugumu wa suala la Mhe. Godbless Lema kuitafuta haki ya dhamana kwa gahrama ya haki za kikatiba kuelekea kuvunjwa, njia ya kupelekea kuipata haki imekua kizingiti ni mtazamo na mapendekezo yetu kuwaa nivema sheria kadhaa zikabadilishwa ili kurahisisha upatikanaji wa haki katika dhamana (Procedures are not Masters of Justice) matakwa ya sheria ya dhamana kwa mujibu wa kifungu cha sheria ya mwenendo wa makosa ya Jinai kifungu cha 148(5) kinaeleza makosa yasiyo dhaminika pia ibara ya 30 ya katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 vingeweza kutumika kunyima dhamana endapo ni kwa maslahi ya umma.

Ikiwa kifungu 148(4) ambacho kimepingwa katika mahakama ya rufani kitaendelea kutumika kabla ya uamuzi basi bado magangano na utata wa wa kisheria; Godbless Lema ni mbunge na lengo la kumtia mtu kizuizini ni ili aweze kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma dhidi yake na si kumuadhibu kabla ya mahakama haijaamua kama ana hatia au laa kwa mujibu wa ibara ya 13(6)b ya katiba ya Tanzania 1977 na kwa mujibu wa kesi ya JAFFER VS REPUBLIC 1997 Hivyo ni vyema sasa kwa kuwa maoni ya jamii (public opinion) yanaona kama haki haitendeki ni vyema pia tukasikia kauli ya msimamizi mkuu wa sheria Tanzania kwa nafasi yake ya kibunge akiwatolea ufafanuzi watanzania kupunguza mijadala na mivutano mikali katika mitandao ya kijamii.
Tunatarajia kwa matumaini makubwa kusikia kutoka kwenu kwaajili ya ustawi wa haki na usawa katika taifa letu.

HITIMISHO.
Uongozi wa Baraza la vijana Taifa, Mikoa na Wilaya ndani ya siku saba, Ikiwa Ben Saanane aliepotea kwa zaidi ya Mwezi mmoja sasa atakua hajapatikana;
Tutalazimika kulipeleka jambo hili zito kwa Mhe. Rais na amiri jeshi mkuu Mhe. J.P Magufuli Ikulu ajue Raia wake amepotea na tutamuomba atoe amri kwa mujibu wa sheria atafutwe mpaka apatikane akiwa mzima na ikiwa vinginevyo pia aagize hatua stahiki zichukuliwe. Itakua pamoja na kumuonesha maeneo ya kutumbua majipu tuliyoyafanyia utafiti na yamebaki kuwa kero kwa Watanzania.

Nawatakia wasaha mwema na Mungu awabariki Msimu huu wa sikukuu
MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE!

Patrobass Katambi
Mwenyekiti Baraza la Vijana Chadema Taifa

CC:
CHRAGG
AG
IGP
TISS
MSAJIRI WA VYAMA VYA SIASA
KUB
M/KITI (TCD)
UONGOZI UKAWA.
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO