NAPE NAUYE AWAPONGEZA TBN KWA UPASHAJI WA HABARI
Dar es Salaam, WAZIRI wa habari na Uenezi, Nape
Nauye, amesema siri ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuingia madarakani ni
mitandao ya kijamii.
Akifunga
kongamano la mkutano mkuu wa Umoja wa Wanachama wa mitandao ya kijamii
(blogeers), Nape alisema CCM imeingia madarakani baada ya kuandikwa kwa upana
mkubwa katika mitandao ya kijamii.
Alisema
mitandao ya kijamii iko na nafasi kubwa katika jamii ambapo asilimia kubwa ya
Watanzania wanatumia mitandao ya kijamii ambapo habari nyingi wakati wa kampeni
walikuwa wakisoma katika mitandao hiyo.
“Leo nitoe
siri kwenu kuwa CCM kuingia madarakani ni ninyi mabloggers, hivyo nawapongezeni
na niko nanyi bega kwa bega” alisema Nauye
Aliitaka
mitandao hiyo kufuata maadili ya upashaji habari na kuepuka upotoshaji jambo
ambalo linaweza kuwa hatari kwa jamii hivyo kuwataka kuzingatia taaluma hiyo.
Mwisho
Waendeshaji wamitandao ya kijamii (bloggers) wakipiga picha ya Selfie na Waziri wa habari na Uenezi mara baada ya kufunga kongamano la mkutano mkuu wa mwaka wa Tanzania Network (TBN) jijini Dar es Salaam leo
0 maoni:
Post a Comment