Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

KCB ARUSHA WATOA MSAADA WA MILIONI 48 KWA TASISI YA ERETO EAST AFRICA


Meneja wa Benki ya KCB tawi la Arusha TFA Hogla Laizer (kulia) akikabidhi Msaada wa hundi ya shilingi milioni 48 kwa mkurugenzi wa shirika la Ereto East Africa foundation Godsave Ole Megiroo.Halfa ya Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ofisi za Benki hiyo zilizopo jijini Arusha
 Meneja wa Benki ya KCB tawi la Arusha TFA Hogla Laizer akizungumza katika
Halfa ya Makabidhiano ya msaada wa hundi ya shilingi milioni 48  kwa shirika la Ereto East Africa foundation.Halfa ya Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ofisi za Benki hiyo zilizopo jijini Arusha.kushoto ni Mkurugenzi wa shirika hilo Godsave Ole Megiroo


 
 
Na Woinde Shizza,Arusha.
 
Benki ya KCB nchini Tanzania imetoa msaada wa kiasi cha fedha cha shilingi Milioni 48 kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya kunawa mikono vinavyojulikana kama Hand washing station  katika shule za Mairowa Intergrity na Kondoa Intergrity zilizoko chini ya taasisi ya  Ereto East Africa Foundation.
 
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika ofisi za benki hiyo  ,Meneja wa Benki hiyo Tawi la Arusha  Hogla Laizer amesema kuwa msaada huo ni moja kati ya mchango wa benki hiyo kwa jamii hususan katika suala la elimu na afya hasa katika maeneo yenye changamoto kubwa ya maji .
 
Meneja huyo amesema kuwa msaada huo tayari umezisaidia shule za Kondoa Intergrity na Mairowa Intergrity zilizoko chini ya Ereto East Africa Foundation .
 
“Katika kuchangia elimu Benki ya KCB kwa kipindi cha miaka mitatu imetoa misaada ya thamani ya shilingi milioni 300 ili kuboresha elimu kwa kutoa madawati na vifaa vingine vya kuboresha huduma za elimu” Alisema Hogla
 
Mkurugenzi wa Taasisi ya Ereto East Africa Foundation Bwana Godsave Ole Megiro amesema kuwa msaada huo utasaidia kutatua tatizo la magonjwa ya matumbo na kipindu pindu yanayotokana na kutokunawa mikono kwa kuanzishwa kwa vituo hivyo vya kunawa mikono.
 
Godsave amesema kuwa wameweka vituo hivyo  karibu na vyoo na karibu na mabwalo ya kunawa mikono jambo ambalo limepunguza idadi kubwa ya wanafunzi waliokuwa wakiugua magonjwa ya matumbo.
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO