Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TAARIFA YA ZIARA YA MH JOSEPH LEONARD HAULE MBUNGE WA JIMBO LA MIKUMI KWENYE KATA ZA KIDODI, ULAYA, NA ZOMBO

ZIARA YA MH JOSEPH LEONARD HAULE MBUNGE WA JIMBO LA MIKUMI KWENYE KATA ZA KIDODI, ULAYA, NA ZOMBO


Jana  Tarehe 21/12/2016 Mbunge wa Jimbo La Mikumi  Mh. Joseph Leonard Haule  aliwatembelea na kuwafariji wahanga  wote ambao nyumba zao zilipatwa na maafa ya mvua zilizoambatana  na upepo mkali mnamo tarehe 17/12/2016 na kupelekea  nyumba 25 kuathirika kwenye vijiji vya Tundu, Msowelo na Iwemba  vilivyopo kata ya Kidodi.

Lakini pia Mbunge wa Jimbo La Mikumi Mh. Joseph Leonard Haule wakati akiendelea na ziara yake ya kuwajulia hali Wahanga, alipata nafasi ya kuhudhuria msiba uliokuwepo ukiendelea maeneo hayo na kutoa  kiasi cha Tsh 50,000 kama rambirambi yake. 

Mara baada ya hapo Mh Mbunge aliagana na wenyeji wake(viongozi wa Kata) na kuendelea na ziara yake Kwenye Kata za Ulaya na Zombo ambapo aliwajulia hali Wahanga wa ugonjwa wa Kipindupindu na kukabidhi vifaa tiba, ambapo Kata Ulaya Mh Mbunge alikabidhi Dripu boksi mbili na glavu boksi moja, ambapo kwa upande wa Kata ya Zombo pia Mh.Mbunge alikabidhi Dripu boksi nne pamoja na boksi moja ya glavu.

SHUKRANI
Mbunge wa jimbo la mikumi Mh.Joseph Leonard Haule anatoa shukrani zake za dhati kwa uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya kilosa pamoja na wadau waliojitokeza kusaidia vifaa tiba kwa ajili ya kunusuru maisha ya wahanga wa ugonjwa wa kipindupindu Kwenye kata za Kisanga,Mhenda,Ulaya,Zombo na Kilangali. Mungu awabariki sana na awazidishie pale mlipojitoa



Imetolewa na:~

Robert A. Galamona
Katibu
Ofisi Ya Mbunge
Mikumi
22/12/2016

Mbunge wa Mikumi akisaini kitabu cha wakeni katika moja ya ofisi za Serikali ya Mtaa Jimboni kwake
Mbunge Joseph Halule na wasaidizi wake wakiwa nyumbani kwa mmoja wa wananchi wenye uhitaji wa msaada


Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO