Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Taswira: Operesheni ya ABIRIA PAZA SAUTI Ilivyofana Jijini Arusha kwa Ushirikiano baina ya Jeshi la Polisi na Mabalozi wa Usalama Barabarani

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, Eng Nuru Selemani akizungumza na vyombo vya habari mapema leo asubuhi wakati wa zoezila ukaguzi wa vyombo vya usafiri na madereva pamoja na elimu kwa abiria kujua haki na wajibu wao wawapo safarini. 
Kamanda Nuru ameeleza kuwa Jeshila Polisi limejipanga vizuri kuhakikisha kwamba wanadhibiti kikamilifu vyanzo vyote na uwezekano wa kutokea kwa ajali zinazozuilika hasa kipindi hiki cha simu wa sikukuu ambapo wasafiri huwa wengi.
Akitoleamfano, amesema mapaka mwakahuu ukiwa unaelekea ukingoni, wameweza kudhibitikwa kiwango kikubwa ajali za mabasi ya abiria jambo ambalo limechangiwa na uamuzi wakuwafikisha maahakamani madereva wazembe tofauti na awali walipokuwa wakiwatoza tu nauli.


Mmoja wa madereva akipimwa iwango cha ulevi kuona yuko kwenye kiwango sahihi kuruhusiwa kuendelea na safari na abiria wake ama la. Zoezi hilo lilifanyika kwa madereva wenginani mmoja tu ndiye aliyepatikanaakiwana kiwango kikubwa cha ulevi na kuondolewa kwenye gari. RTO Arusha, Eng Nuru Seemani akishuka kutoka kwenye gari baada ya kufanya ukaguzi

Kamanda kwa Kikosi cha usalama Barabarani Eng Nuru Selemai(katikati) akifafanua jambo kwa vijana wake


Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, Eg. Nuru Selemani akielekeza masuala mablimbali na kujibu maswali ya abiria na wasafirishaji katika eneola Stand Kuu ya mabasi Arusha mapema leo asubuhi

Mabalozi wa Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha wakiwa eneola standakuu ya Mabasi yanayotoka nje ya Arusha mapemaleo asubuhi katika pilikapilika za kuendesha zoezilakutoa elimu kwa abiria kuhusiana na masualammbalimbali ya wajibu na haki za abiria kwa lengola kuhakikisha safari inakuwa salama. Kutoka kushotoni makamu Mwenyekiti Bakari Msangi anafuatiwana Balozi Vero Ignatus na kisha Mweyekiti Stellah Rutaguza


Mmmoja wa wasafirishaji abiria akihojiwana waandishiwa habari na kuelezea baadhi ya changamotona kero wanazokutana nazo toka kwa abiria safarini ikiwemo malalamiko ya abiria kudhani garini bovu pale linapotembea kwa kikomo cha spidi 80 kwa saa. (80km/hr) 

Mwenyekiti wa Mabalozi wa Usalama barabarani (RSA) Mkoa wa Arusha, bI Stellah Rutaguza akitoa ufafanuzi kwa mwakilishi wa wakata tiketi za abiria Stendi Kuu Arusha.

Makamu Mweyekiti wa RSA, BakariMsangi akifafanua jambo kwa wadau wa usafiri na usafirishaji
Baadhi ya picha za pamoja baina ya Askari wa usalama wa Barabarani na Mabalozi wa usalama Barabarani kutoka Taasisi ya kiraia ya RSA

Balozi wa RSA Vero Ignatus akishuka kwa tahadhari kutoka kwenye moja ya mabasi mara baada ya kutoa elimu na basi hilo kukaguliwa na kuruhusiwa kuondoka.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO