Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

"Kesi ya UKUTA" waliyofunguliwa Madiwani wa CHADEMA Siha Yafutwa na Mahakama

Taarifa tuliyopokea kutoka Siha inaeleza kuwa kesi Na. 86 ya mwaka 2016 iliyokuwa ikiwakabili Katibu wa CHADEMA Jimbo la Siha, Emanuel Nabora, madiwani wawili wa chama hicho Mh Jackson Rabo Diwani wa Kata ya Ndumeti na  Diwani wa Viti maalum Bi. Witness Nerey Riwa imefutwa  Mahakama ya Wilaya ya Siha chini ya uamuzi wa Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Mheshimiwa Anold Kirekiano baada ya kuridhika na hoja za upande wa utetezi kuomba kesi hiyo ifutwe kutoka na na dosari za kisheria katika hati ya mashitaka.
Kesì hiyo ilisomwa kwa mara ya kwanza tarehe 31.8.2016 ikiwa na makosa mawili kwa watuhumiwa wote watatu ambapo kosa la kwanza liliwahusu watuhumiwa wote watatu kwa pamoja na watuhumiwa wengine ambao walikuwa bado wanatafutwa, kwamba walikula njama kinyume cha sheria ya kanuni za adhabu namba 16 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002 kifungu cha 385 ambapo ilielezwa kwamba mnamo tarehe 24.8.2016 majira ya saa 4.30 huko Sanya Juu Wilaya ya Siha watuhumiwa hao wote walikula njama na kufanya kusanyiko lisilokuwa halali kinyume cha sheria.
Kosa la pili liliwahusu pia watuhumiwa wote kwa pamoja wakidaiwa kufanya kusanyiko lisilokuwa halali kinyume cha sheria ambapo ilielezwa kwamba washitakiwa wote pamoja na wengine ambao hawajakamatwa  mnamo tarehe 24.8.2016 majira ya saa 4.30 asubuhi huko Sanya juu Wilaya Siha baada ya kula njama walifanya kusanyiko lisilo halali kwa lengo la kuwashawishi watu kufanya uaasi (unlawfull assembly with intent to influnce people to protest).
Baada ya watuhumiwa kusomewa mashitaka hayo wakili wa upande wa utetezi wakili msomi ELIA J KIWIA aliweka pingamizi la awali kwamba maelezo ya kosa yaliyotolewa hayana maelezo muhimu  ambayo yangewezesha upande wa Jamuhuri kutengeneza kosa dhidi ya viongozi hao kamasheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kifungu cha 132 kinavyoeleza na hivyo kuiomba Mahakama hiyo kuitupilia mbali kesi hiyo na kuwaachia huru watuhumiwa hao.
Katika kutoa ufafanuzi wa hoja yake hiyo, Wakili wa upande wa utetezi alitumia sheria mbalimbali, vitabu, kamusi na rejea ya kesi za mahakama ya rufani zilizokuwa zikitoa muongozo, akisema kwamba lengo la kifungu hicho cha sheria halikuwa kuzuia uasi bali ilikuwa ni kuzuia makusanyiko yote ambayo yataogopesha watu na kusababisha uvunjivu wa amani au kusababisha watu wakasirike na kusababisha uvunjifu wa amani.
Wakili Kiwia aliieleza Mhakama kwamba kwa jinsi maelezo ya kosa yalivyowasilishwa wateja wake hakuwa na kosa lolote walilokuwa wametenda bali ilionekana Jamuhuri walikuwa wametengeneza kosa jipya ambalo halipo kisheria.
Upande wa Jamuhuri ulikuwa ukisisitiza kuwa maandalizi ya hati hiyo ya mashitaka ilikuwa sahihi.
Kutoka kushoto Mh Jackson Rabo Diwani wa Kata ys Ndumeti, Wakili msomi Elia Kiwia, Diwani Viti Maalum Siha Witness Narei Riwa na mwisho ni Emmanuel Nabora, Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Siha


Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO