Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mh Kalisti Lazaro Bukhay akimpongeza na kumpatia cheti cha shukrani Mkurugenzi wa kampuni ya Achieve in Africa Mh Alex Marti kwa kusaidia kufadhili sare za shule kwa watoto 400 wanaoishi katika mazingira magumu, kusaidia ujenzi wa madarasa 11 na madawati 280 shule ya msingi Olasiti ambayo inasimamiwa na Halmashauri ya Jiji.
Achieve in Africa imesaidia pia upatikanaji wa madawati 60 na ujenzi wa matundu 20 ya choo kwa shule ya sekondari Olasiti.
Mh Kalisti amempongeza mkurugenzi huyo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Olasiti kupitia CHADEMA na kumkabidhi cheti kama tuzo maalumu katika ofisi ya Meya kwa niaba ya taasisi ya Achive in Africa kupongeza juhudi binafsi za diwani huyo na taasisi hiyo kuisaidiana na Halmashauri ya Jiji kutatua changamoto zinazoikabili jamii ya Arusha nje na bajeti rasmi iliyotengwa na Halmashsuri.
Baadhi ya majengo ya madarasa na vyoo yanaendelea kumaliziwa ujenzi wake na na Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Diwani wa Kata ya Olasiti Jijini Arusha kupitia CHADEMA, Mh Alex Mart (kulia) akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Meya wa Jiji la Arusha ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Sokoni I, Mh Kalisti Lazaro Bukhay |
0 maoni:
Post a Comment