Mbunge wa Rombo Mh Joseph Selasini (CHADEMA) ataongoza mamia ya vijana na wanajamii wengine katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti jimboni humo kesho January 1, 2017 katika eneo la Mamsera.
Zaidi ya miche 1000 ya miti imeandaliwa kuoteshwa maeneo mbalimbali ya Jimbo la Rombo katika jitihada za kukabiliana na uharibifu wa mazingira kutokana na ukame uliotokana na tabia ya wananchi kukata miti bila kuotesha miti mbafala.
Zoezi hilo linatarajiwa kuhitimishwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mh Agnes Hokororo eneo la Mkuu yalipo makao makuu ya kiutawala ya Wilaya ya Rombo.
Picha ya Maktaba: Mbunge wa Rombo Mh Joseph Selasini akikagua athari za mvua mwaka jana kati Wilaya yake ya Rombo. Picha: www.brotherdanny.com |
Wilaya ya Rombo ambayo kijiografia ndiko ulipo mlima Kilimanjaro imeathirika sana na mabadiliko ya tabia nchi kiasi cha kufikia kukauka kwa vijito na chemchemi nyingi na kupelekea adha kubwa ya upatikanaji maji tofauti na zamani.
Wenyeji wameiekeza blogu hii kuwa joto limeongezeka sana na mvua hazitabiriki tena huku theluji mlimani ambayo husababishwa na unyevu nyevu wa miti kwenda mlimani inayeyuka.
Mh Mbunge anawakaribisha watu wote kushiriki kampeni hii muhimu kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo
0 maoni:
Post a Comment