Na.Vero Ignatus
Arusha.
Mabalozi
wa usalama wa usalama barabarani kwa kushirikiana na jeshi la polisi
kikosi cha usalama barabarani wamefanya zowezi la kutoa elimu kwa
abiria pamoja na madereva huku jeshi la polisi wakiwapima madereva
ulevi na kukagua ubora wa magari hayo kabla ya kuanza safari kuelekea
mikoani
Zowezi
hilo limeongozwa na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani SSP Nuru
Suleiman na katika stendi kuu ya mabasi yaendendayo mikoani na nchini
jirani Jijini Arusha huku zowezi hilo likiwa na lengo la
kuelimisha,kukemea na kuripoti mwenendo mzima unaokiuka sheria za
usalama barabarani.
Kwa
upande wake Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Nuru
Suleiman amesema kuwa kampeni hiyo inamafanikio makubwa tangia
ianze kwenye wiki ya nenda kwa usalama kwani tangia mwanzoni mwa mwaka
2016 hakuna ajali ya basi iliyotokea na kuleta madhara kwa jamii kwa
ujumla.
"Kwakweli
tunamshukuru sana Mungu kwani tangia mwaka huu uanze hatujapata ajali
ya basi inaonyesha madereva wamepata elimu na wanaitendea kazi na
tunawaomba waendelee kuwa makini ili ajali ikiwezekana zisitokee
kabisa "alisisitiza kamanda Nuru.
Aidha
amesema kuwa wamekuwa wakiwapima madereva ulevi na madereva ambao
wanakiuka sheria za usalama barabarani na pale wanapogundulika na
makosa wapo wengine wanalipishwa faini na wengine wanapelekwa
mahakamanikufutiwa leseni na kuzuiliwa kuendesha chombo cha moto
kabisa.
Kwa
upande wake makamu mwenyekiti wa mabalozi wa usalama barabarani Bakari Msangi
amesema kuwa lengo kubwa la oparesheni abiria paza sauti ni
abiria kutambua wajibu na haki yake awapo ndani ya chombo cha usafiri
ikiwemo kutokukaa kimya pale anapomuona dereva anakwenda kinyume na
sheria za usalama barabarani,ulevi,kuyapita magari mengine mahali
ambapo hapastahili,kutoa lugha zenye utata kwa abiria,dereva kuongea
na simu wakati anaendesha,yote haya anatakiwa kutoa taarifa kwa jeshi
la polisi.
Aidha amesema
kuwa
abiria anatakiwakutoa taarifa pale dereva anapokuwa kwenye mwendo
kasi, kufunga mkanda awapo ndani ya gari ili kwamba kama imetokea
dharura yeyote asiweze kuhamishwa kwenye kiti alichokaa,pia wawapatie jeshi
la polishi ushirikiano kwaajili ya usalama
zaidi.
"Unajua abiria
wengine ni chanzo cha ajali kwani wanakuwa wanamchochea
dereva
kuendesha kwa mwendo kasi,wanapoulizwa na askari hawasemi kama
kuna
tatiuzo hilo ni kosa hebu wapeni ushirikiano jeshi la polisi kikosi
cha usalama barabarani ni kwaajili ya faida yenu jamani."alisisitiza
Bakari
Naye mwenyekiti
wa usalama barabarani Jijini Arusha bi.Stella Rutaguza amesema
kuwa
kazi
kubwa abiria kutokukaa kimya pale anapomuona
dereva anakiuka sheria za usalama barabarani ili kuweza kuepuka
ajali ambazo zinaepukika.
Amesema
zowezi hili la Operesheni Abiria Paza Sauti litaendelea hadi
April 2017.
Mkuu wa kikosi cha
Usalama barabarani SSP Nuru Suleiman akiwa katika kituo cha kikuu cha
mabasi yaendayo mkoania na nchi jirani ,mkoani Arusha tayari kwa kutoa
elimu kwa abiria na madereva leo 19Desemba 2016.Picha pamoja na habari
na Vero Ignatus Blog.
Kutoka kushoto ni mwenyekiti wa Usalama barabarani mkoa wa Arusha bi.Stella Ruraguza akizungumza na mwenyekiti wa wakata tiketi stendi kuu ya mabasi yaendayo mkoani na nchi jirani Babuu Jumanne .Picha pamoja na habari na Vero Ignatus Blog |
| ||
Wa kwanza kushoto ni koplo Athilio Choga aliyepo katikati ni Vehicle Inspector Koplo Songoi na wa kwanza kulia ni PC Rajabu |
0 maoni:
Post a Comment