Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: SHAKA WA UVCCM AKIONGOZA JOGGING YA VIJANA MKOANI KAGERA BAADA YA UZINDUZI KARAGWE

 Kaimu katibu mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka wa katikati akiendeleza
zoezi la jogging pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM  Wa Uvccm Mkoa wa Karagwe
Ndg Yahaya Kateme wa kwanza kushoto.


Ndugu Shaka H.Shaka juzi alizindua rasmi kampeni
ya Jogging UVCCM yenye kauli mbiu ya 'MAZOEZI KWA AFYA' iliyozinduliwa
Kitaifa Wilayani Karagwe.

Katika Mazozi hayo Kaimu katibu mkuu ameshiriki
jogging na Mazoezi Viungo akiongozwa na Mwenyekiti  Uvccm mkoa wa Kagera
ndg YAHYA KATEME,Mkuu wa Wilaya Karagwe  Mhe. Godfrey Ayub  Mheluka pamoja
na vijana na viongozi mbalimbali  Wa Chama na Serikali Wilayani humo.

Akiongea mara baada ya Mazoezi hayo Ndg: kaimu katibu mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu
Shaka amewataka Makatibu wa UVCCM Ngazi za Wilaya Nchini kote kuzingatia
maelekezo yaliyotolewa tangu Mnamo tarehe 24 Mwezi Oktoba 2016 la kuanzisha
jogging Club alisema "nitumie fursa hii kuwapongeza sana kwa kutambua
umuhimu wa mazoezi, sasa Vijana lazima wawe wakakamavu na tayari muda wote
hatuwezi kuwa na taifa la vijana goigoi wasio jiweza kama ambavyo  hata
makamu wa Rais alivyounga mkono katika swala hili la mazoezi " 

Pia amewataka vijana wote kushiriki ipasavyo Zoezi hili amesema '' Jogging ni
swala muhimu sana kwa vijana kwani pamoja na kujenga miili yetu jogging
itatufanya tuwe wamoja t wenye ushirikiano wa kudumu haswa katika mambo
mbali mbali ya kijamii''. 

Kaimu katibu mkuu huyo yupo katika ziara ya siku nane
mkoani Kagera ambapo atatembelea wilaya zote 8 za mkoa wa Kagera.

 Kaimu katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka wa pili kulia akiendelea
na Zoezi la Unyooshaji wa Viungo pamoja na Mkuu wa Mkuu wa Wilaya ya
Karagwe Mhe. Godfrey Ayub  Mheluka


 Kaimu katibu Mkuu Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi Taifa Shaka Hamdu
Shaka akiruka Mchaka mchaka katika viwanja vya CCM Wilaya ya karangwe juzi.


CHANZO -PICHA NA MAELEZO: WOINDE SHIZA
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO