Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Halmashauri ya Jiji la Arusha Imesaini Makubaliano ya Kibiashara na Jimbo la Hubei China


Halmashauri ya Jiji la Arusha imesaini makubaliano na Jimbo la Hubei nchini China ili kuwasaidia jiji hilo katika nyanja za kilimo, biashara, sayansi na teknolojia.

Akizungumza mara baada ya kuingia makubaliano hayo leo, Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro amesema makubaliano hayo ni ya mwaka mmoja na yanatarajia kufungua fursa mbalimbali za kibiashara baina ya pande zote mbili.

Mkurugenzi wa jiji la Arusha, Athuman Kihamia amesema wanalenga Arusha kuwa miongoni mwa majiji bora kibiashara na hivyo makubaliano hayo yatasaidia wafanyabiashara jijini hapa kufungua milango ya kibiashara na jimbo la Huangshi nchini China.

Makamu mwenyekiti wa kamati maalumu ya Bunge la Huangshi nchini China, Weng Bin alisema mbali na biashara, makubaliano hayo yatafungua fursa mbalimbali kwa walimu wanaofundisha lugha ya Kiswahili mkoani Arusha kwenda kufundisha nchini China.
Source:Mwananchi, Jumamosi Disemba 16, 2026
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO