Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

DARASA AISIMAMISHA ILALA KWA MAANDALIZI YA SHOO KALI DARLIVE JUMAMOSI HII





MWANAMUZIKI wa Hip Hop anayefanya poa kwa sasa hapa Bongo, Shariff Thabeet ‘Darassa’, leo amefanikiwa kuisimamisha Ilala alipokutana na mashabiki wake kabla ya Jumamosi hii hajapanda kwenye Jukwaa la Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam.

Darassa na Roma, kwa pamoja watapanda katika Jukwaa la Dar Live kwenye Mkesha wa Mwaka Mpya ili kumaliza ubishi wa nani mkali wa michano katika pambano la Nichane Nikuchane.

Akiwa kwenye Viwanja vya Karume jijini Dar, leo, Darassa aliisimamisha Ilala pale alipotoa burudani fupi ikiwa ni kionjo kabla ya shoo yenyewe kamili ya siku hiyo.

Akizungumza na mashabiki wake, Darassa alisema: “Mashabiki zangu, siku hiyo ya Mkesha wa Mwaka Mpya mnachotakiwa kufanya ni kuja kwa wingi pale Dar Live kushuhudia miujiza nitakayoifanya kwani siku zote naamini huwa nafanya miujiza kila ninapopanda jukwaani.”

Naye Meneja wa Global Publishers ambao ni waandaaji wa pambano hilo, Abdallah Mrisho, alisema: “Shoo hii inayoenda kufanyika ni ya tofauti, kama tujuavyo R.O.M.A na Darassa kwa sasa ndiyo habari ya mjini hasa kwenye Muziki wa Hip Hop, hii ni mara ya kwanza kwa Darassa kupanda kwenye Jukwaa la Dar Live, hivyo mashabiki ni fursa yenu kujumuika naye siku hiyo.”

Katika hatua nyingine, Meneja wa Dar Live na mratibu wa mpambano huo, Juma Mbizo, alisema: “Kwa kiingilio cha Sh 5,000, mashabiki watapata fursa ya kuingia na kushuhudia mpambano huo mkali ambao rasmi utaanza saa 7 mchana mpaka majogoo.”

Mbali na wakali hao kupanda jukwaani siku hiyo, pia wengine watakaotoa burudani ni pamoja na Kundi la Muziki wa Taarab la Jahazi, Juma Nature, Makhirikhiri, MC Darada, Topido, ID Classic, H-Mbizo na wengine wengi.

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO