Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Tanzania Centre for Democracy (TCD) yawakutanisha pamoja CCM, CHADEMA na Jeshi la Polisi Arusha Mjini

Picha ya pamoja ya viongozi waliojumukika katika kikao hicho cha majadiliano
Katibu wa Baraza la Wanawake CHADEMA Arusha Mjini ambaye pia ni Diwani wa Viti Maalumu katika Baraza la Halmashsuri ya Jiji la Arusha, Mh Happy Charles akizungumza katika kikao hicho,
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA Arusha Mjini ambaye pia ni Naibu Meya wa Hlamashsuri ya Jiji la Arusha Mh Viola Likindikoki akizungumza
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha na Katibu wa chama hicho Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa akiongea katika kikao hicho
Kituo cha Demokrasia Tanzania (Tanzania Centre for Democracy-TCD) jana tarehe 19/12/206 kiliwakutanisha viongozi wa vyama vya siasa  kutoka Wilaya ya Arusha Mjini, Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Polisi wa Wilaya - OCD pamoja na madiwani wanaounda Halmashauri ya Jiji la Arusha katika semina ya pamoja kwa nia ya kuimarisha mahusiano katika kuutumikia umma bila tofauti za kisiasa.

Taasisi hiyo inayoundwa na vyama vya siasa vyenye uwakilishi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (CHADEMA, CCM, CUF, NCCR Mageuzi na ACT) huku vyama visivyo na uwakilishi bungeni vikiwa wanchama washiriki.

TCD ina mfumo ambapo vyama vishiriki huchagua chama kimoja kuwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti kwa kipindi cha mzunguko wa miezi sita ambapo kwa sasa Mwenyekiti wa TCD ni Mhe Freeman Mbowe (CHADEMA) ambapo kwa kikao cha jana aliwakilishwa na Katibu wa chama hicho Kanda ya Kaskazini ambaye  pia ni Mwenyeki wa chama Mkoa wa Arusha, Mh. Amani Golugwa.

Katika semina hiyo viongozi wa vyama vya siasa wilayani hapa walifanikiwa kuunda Jukwaa la Majadiliano ya vyama vya siasa ambapo walimchagua Mhe.Derick Magoma ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Arusha Mjini kuwa Mwenyekiti wa Jukwaa hilo na Ndugu Idd Mpengo (Katibu wa UVCCM - Arusha Mjini) kuwa katibu wa Jukwaa hilo.

Aidha TCD inafanya kazi kwa malengo ya kuimarisha mazungumzo baina ya vyama vya siasa kwa kuendesha majadiliano kwa viongozi wa vyama vya siasa ngazi ya Taifa hadi ngazi za chini ambapo kwa sasa imeanzisha majukwaa haya ya majadiliano ya vyama vyenye madiwani kwenye ngazi ya Wilaya.

Picha na Maelezo: Mozec Joseph
Afisa habari CHADEMA - Kanda ya Kaskazini
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO