Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Bonanza la Wazee Arusha lafana!

1 Jumapili hii kulikuwa na bonanza la mchezo wa mpira wa miguu hapa Arusha ambapo timu ya Arusha Wazee Sports Club iliialika timu ya Bunge la Kenya kwenye mchezo wa kirafiki. Timu nyingine mbili za Bunge la Afrika Mashariki na TGT Arusha zilishiriki bonanza hilo ambapo timu ya Arusha Wazee iliibuka kidedea na kujinyakulia kombe baada ya kuwafunga Wabunge wa Kenya 5-3 kwa mikwaju ya penalt. Baada ya hapo kukafanyika tafrija kubwa ya msosi na vinywaji pamoja na muziki uwanjani hapohapo. Shukrani ziwaendee Bunge la Afrika Mashariki, TBL na Tanzania Distilleries Ltd walioshirikiana na Wazee kufadhili bonanza hilo, Bunge la Kenya sasa limeialika timu ya Wazee Arusha kwenda Mombasa kwa ziara ya kirafiki ya kimichezo mwishoni mwa mwezi wa Agosti wakati wa Mombasa Agricultural Show ili kuimrisha ushirikiano ndano ya Jumiya ya Afrika Mashariki (Picha na Maelezo: Mjengwa Blog)

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO