Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MOVEMENT FOR CHANGE NDANI YA DAR ES SALAAM JUMAMOSI MEI 26

DSCN0501Moja ya mikutano ya CHADEMA Mkoani Arusha, hapa wakiitikia salamu ya “Peoples Power”

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatarajiwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhaara katika viwanja vya Jangwani Jijini Dar es Salaam, Jumamosi ya tarehe 26/5/2012 Jumamosi ambapo Mwenyekiti wa chama hicho taifa Mh Freeman Mbowe, na Katibu Mkuu wake Dr Wilbroad Slaa na viongozi wa kitaifa na wabunge wa chadema watahutubia.

Mkutano huo unaelezwa kuwa ni utangulizi wa ziara ya oparesheni ya chama kujiimarisha mikoa ya Lindi na Mtwara inayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 27 Mei 2012.

James Millya na Ally Banaga, na baadhi ya waliokuwa viongozi wa CCM hapo awali na kuamua kujiunga na CHADEMA hivi karibuni katika operesheni ndogo waliyoibatiza jina la “Vua Gamba Vaa Gwanda” watakuwepo katika mkutano huo.

Hukumu Kesi ya Mnyika keshokutwa

Katika hatua nyingine, hukumu ya kesi ya kupinga Ubunge wa Mh John Mnyika inararajiwa kujlikana Mei 24 ambapo Mbunge huyo amewataka wananchi na wapenzi wake kufika kwa wingi kusikiliza hukumu dhidi ya kura zao.

Kwa mujibu wa blog ya Mh Mnyika, kutakuwa na kile alichoita  ‘get together bottle party’ siku hiyo hiyo baada ya hukumu kwa gharama binafsi.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO