Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mwanakijiji - Shibuda anafanya nini CHADEMA?

Hii ni tafakuri ya MM Mwanakijiji, Administrator wa mtandao wa Jamii Forum katika bandiko lake leo

John-Shibuda

Mh John Shibuda, Mbunge wa Maswa Mashariki (CHADEMA)

Mwanankijiji anaanza hivi.. “Ukiwa na askari katika kikosi chako ambaye anaamini majeshi ya adui ni bora zaidi na yanastahili kushinda vita askari huyo anakuwa ni msaliti na anapofanya kazi au jitihada ya kutaka adui ashinde kijeshi huo ni uhaini. Shibuda kutangaza kuwa anataka kugombea Urais kupitia CDM mwaka 2015 siyo tatizo.

Hata hivyo anapofika mahali kuisifia CCM na kuiona kuwa haina mbadala anakuwa amevuka mpaka wa kisiasa kwani inaonekana mapenzi na imani yake iko kwa CCM. Kama hili ni kweli - na nimewahi kusema mahali pengine - basi ni wakati wa kumsaidia Shibuda kuondoka CDM hata kwa gharama ya kupoteza jimbo lake la Maswa Mashariki.

Hii ni kwa sababu mpinzani ambaye anaamini kuwa tatizo la Tanzania siyo kushindwa kwa sera za CCM bali ni watu wachache CCM na kuwa sera za CCM ni bora zaidi anastahili kwenda CCM ambako yeye kama mtu mzuri anaweza kupewa nafasi ya kuzitekeleza hizi sera anazozipenda.

Kama Shibuda au mtu mwingine yeyote kwenye upinzani anaamini sera za CCM ni bora na zinafaa kuliinua taifa basi anayo haki - na sababu - ya kuamua kujitoa upinzani kwenda CCM ili akapewe nafasi ya kuzitekeleza sera hizo.
Kama hatoondoka mwenyewe basi uongozi wa chama unapaswa kumvua uanachama mara moja kwani atakuwa ameenda kinyume kabisa na msingi wa chama”

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO