Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mh Selasini anahitaji maombi yako, hali yake na majeruhi wengine bado sio nzuri

ajali ya Selasini Hii ndio picha halisi ya gari ya Mh Selasini baada ya ajali iliyopelekea vifo vya watu watatu hapo hapo, akiwemo mama yake mzazi, iliyotokea eneo la Bomang’ombe Moshi Mei 24 Mwaka huu (Picha na Zion William, Program Manager at PIPPI Foundation)

Hali ya kiafya ya Mbunge wa Rombo (Joseph Selasini) alielazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC kufuatia ajali ya gari iliyomtokea Mei 24, 2012 katika eneo la Boman’gombe Wilayani Hai inaelezwa kuwa bado haijaimarika.

Taarifa zinaeleza kuwa Mbunge huyo bado anahisi maumivu makali sehemu za kifuani, lakini majeraha ya mikononi yameanza kuonesha nafuu ya kupona.

Mke wake ambae pia walipata ajali hiyo iliyopelekea vifo vya mama mzazi wa mbunge, mama mkwe wake na ndugu mwingine hapo hapo, yeye bado yuko amelazwa katika chumba cha watu mahututi kwa uangalizi zaidi na hali yake inaelezwa kuwa sio nzuri.

Katika hatua nyingine, inalelezwa kuwa maziko ya marehemu mama mzazi wa mbunge huyo yanatarajiwa kufanyika katika kijiji cha Kiria – Makidi Wilayani Rombo siku ya Jumatano Mei 30, 2012.

Wakati huo huo baba mzazi wa mbunge huyo nae amelazwa hospitalini hapo kwa matatizo ya kupooza mwili.

Blog hii inawaomba watanzania kufanya maombi kumuomba Mungu kunusuru afya na uhai wa majeruhi hawa na halikdhalika kumpa ujasiri Mbunge huyu katika kipindi hiki kigumu kwake, na pia kwa wafiwa wote.

Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi, na awapatie uponaji wa haraka majeruhi wote ili waweze kuendelea na shughuli zao za kulitumiia taifa. Amina!

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO