Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Nassari, Lema wadai kutishiwa kifo

SIKU chache baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kata ya Usa River, Jimbo la Arumeru Mashariki, Msafiri Mbwambo (36), kuuawa kwa kuchinjwa Aprili 27 mwaka huu, Mbunge wa Jimbo hilo, Joshua Nassari na baadhi ya viongozi wa chama hicho, wamedai kupokea ujumbe wa maneno kwenye simu ya kiganjani unaowatishia kuwaua.

Akizungumza mjini hapa, Nassari alisema amepata ujumbe wa kumtishia kumuua na viongozi wa matawi wa jimbo la Arumeru Mashariki ambao walikuwa mstari wa mbele kumpigania kupata ushindi kwenye kampeni.

Alisema ujumbe huo aliupata kupitia simu yenye namba 0753-211 367, ambapo namba hiyo ilituma ujumbe wa kuwatishia kuwachinja, kwa aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, Mwenyekiti wa Wilaya ya Arumeru, Gadiel Mwanda, Katibu wa Wilaya hiyo, Totinan Ndonde.

Mwenyekiti wa Kata ya Seela Sing’isi, Simba Kimunto na aliyekuwa Mkuu wa operesheni ya ushindi wake, John Mrema.
Nassari alisoma ujumbe huo kuwa ni, “Tumekuona unabeba jeneza kwenye gazeti, tunakuhakikishia utabeba majeneza Arumeru Mashariki, mpaka ukimbie Ubunge na baada ya Mwenyekiti Usa (Msafiri Mbwambo) kumchinja, sasa ni Simba Kimunto muda usiojulikana, utabeba jeneza lake, Jimbo hili tutalichakaza ndani ya miezi sita, nakutakia mazishi mema ya mfululizo.”

Alisema kuwa baada ya kupokea ujumbe huo akiwa anausoma ukaingia ujumbe mwingine kwa namba hiyo hiyo ukisema, “Bado wewe na Wenyeviti Chadema kwenye kata zako,”

Nassari alisema kuwa mtu huyo asiyejulikana alituma ujumbe kwa Godbless Lema usemao, “Wewe ng’ombe kama Kimunto alikuwekea Wameru 300 kukulinda Arumeru, sasa wewe utamwekea Wachaga wangapi?

Kwa sababu baada ya m/kiti Usa River tunamchinja yeye.” Alisema Lema naye akiwa
anatafakari ujumbe huo uliingia mwingine ukisema,” Baada ya Mwenyekiti wako wa Usa atafuata Mwenyekiti wa kata ya Seela-Sing’isi Samba Kimunto huyu amekuwa kero wilaya hii ya Arumeru Wenyeviti wa Jimbo hili tutakabiliana nao mwezi huu mtamzika sambamba Kimunto unalo la kusema.”

Aidha alisema kuwa baada ya kupata ujumbe huo alifanya mawasiliano na Katibu wa chama chake wa wilaya hiyo, Totinan Ndonde, ambaye alikwenda kituo cha Polisi cha wilaya hiyo, kutoa taarifa na alipewa RB yenye namba USR/RB/1671/2012.

Naye Katibu wa Wilaya ya Arumeru, Totinan Ndonde alipopigiwa simu kuulizwa kuhusiana na hilo, alikiri kupokea ujumbe huo wa vitisho vya kuuliwa na wenyeviti wake wa kata na akatoa taarifa Polisi kwa Kaimu Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya hiyo, John Marona kupewa RB namba USR/RB/1671/2012.

Chanzo: Habari Leo, Mei 4, 2012

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO