Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Leticia Nyerere kushitaki waliomkashifu

MBUNGE wa Viti Maalum, Leticia Nyerere (CHADEMA), ametishia kuwashitaki watu waliotoa taarifa katika vyombo vya habari, zikidai kuwa alikuwa amekamatwa na polisi kuhusiana na makosa aliyotenda nchini Marekani.

Katika taarifa yake jana kwa vyombo vya habari, Leticia alieleza kusikitishwa kwake na taarifa hizo, akidai kuwa zimemdhalilisha na kumkashifu mbele ya jamii inayomheshimu na kumthamini, na hivyo atachukua hatua za kusafisha jina lake.

Alisema tuhuma hizo zilizosambazwa katika moja ya mitandao hapa nchini na kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari, Mei 14, mwaka huu, zilikuwa za kutungwa, na zilizolenga kumchafua mbele ya Watanzania waishio Marekani na hapa nchini.

Mbunge huyo alisema tayari ametoa taarifa kwa mamlaka za kisheria nchini Marekani, na tayari uchunguzi utaanza kuwanasa wale wote waliohusika kusambaza uzushi huo.

Mei 14, mwaka huu, mtu aliyejitambulisha kama Amos Cherehani, akidai kuwa Katibu wa CHADEMA, tawi la Marekani, alisambaza taarifa za kukamatwa kwa mbunge huyo jijini Washington DC, kwa tuhuma za kutenda makosa mawili ya jinai, likiwemo la kujipatia kadi ya kijani (Green Card) kwa njia ya udanganyifu.

Aidha, Cherehani ambaye alikuwa akiwaomba Watanzania kumchangia mbunge huyo fedha za kukabiliana na kesi hiyo, alisema anatuhumiwa kufanya kosa la kuvunja masharti ya dhamana, kwa kutofika mahakamani hapo Februari 10, mwaka huu, katika kile kilichosemwa ni kesi ya kutapeli dola 15,000 toka kwa mtu aliyetajwa kama dada Cooper.

Hata hivyo, taarifa hizo zilikanushwa vikali na Leticia mwenyewe, na baadhi ya viongozi waandamizi wa CHADEMA, ambao walimtaka atoe maelezo ya kujisafisha kwa Watanzania.

Wakati huo huo, mbunge huyo, amesema kuwa, uzinduzi wa tawi la CHADEMA katika mji wa Maryland nchini Marekani, utafanyika Mei 27.

Chanzo: Tanzania Daima

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO