Hawa ni baadhi ya wafuasi wa CHADEMA waliojitokeza katika viwanja hivyo Aprili 7 mwaka huu kusikiliza tamko la chama baada ya Mahakama Kuu kutengua matokeo yaliyompa Ubunge Mh Lema.
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatarajia kufanya mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya NMC , Jijini Arusha.
Mkutano huo utahutubiwa na Mwenyekiti wa chama hicho ambae pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzania Bungeni, Mh Freeman Mbowe pamoja na aliekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema ambae amekuwa akitumiwa na chama chake katika programmu yao mpya maarufu kama “Movement for Change” akizunguka nchi nzima kuhamasisha mabadiliko tangu Mahakama Kuu Kanand ya Arusha itengue ubunge wake Aprili 5 mwaka huu.
Pamoja na mambo mengine, mkutano huo utawatambulisha wanasiasa wapya waliohamia chama hicho.
Tangia jana habari za kuwako kwa mkutano huo zimekuwa gumzo miongoni mwa wananchi hali inayohisiwa kukusanya watu wengi kuliko mikutano iliyotangulia. Wasiwasi huu ndio ulipelekea watu wasiojulikana kupita na gari mitaani wakitangaza kuwa kutakuwa na vurugu na kwamba Lema ameandaa watu wakavamie maduka ya watu baada ya mkutano.
Blog hii inaamini Jeshi la Polisi liko makini na litawachukulia hatua wale wote watakaojihusisha na vitendo vya vurugu bila kujali ni nani amewaandaa.
Mkutano huwo utakuwa live kupitia blog hii na website ya Arusha Mambo www.arushamambo.com kuanzia saa saba mchana.
0 maoni:
Post a Comment