Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

AJALI MBAYA JIONI HII: MBUNGE WA ROMBO ANUSURIKA KIFO, WATATU WAFARIKI PAPO HAPO AKIWEMO MAMA YAKE

selasini Tumepokea taarifa ya ajali mbaya ya barabarani jioni hii ikieleza kuwa Mbunge wa Rombo (CHADEMA), Mh Joseph Selasini (pichani) pamoja na watu wengine 5 wamepata ajali mbaya eneo la Bomang’ombe, Wilayani Hai, Kilimanjaro, ambapo watu watatu kati ya sita wamekufa hapo hapo akiwemo mama  mzazi wa mbunge.

Taarifa pia imethibitishwa na Mh Selasini mwenyewe kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Facebook ambapo ameandika “Tumepata Ajali Mbaya Muda Si Mrefu. Maombi yenu Tafadhali Makamanda.”

Kwa mujibu wa vyanzo vya taarifa hiyo, inaelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendesha baiskeli ambae alikuwa ameingia barabarani, na ndipo Mh Selasini alipojaribu kumkwepa gari ikahama njia na kuingia mtaraoni.

Selasini alikuwa pia ameambatana na mke wake, Digna Kavishe ambae amenusurika kifo, lakini amejeruhiwa na kukimbizwa hospitali ya Bomang’ombe.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO