Mjasiriamali huyu ameweka kituo chake jirani na Soko Kuu Arusha. Bidhaa anazozalisha ni kama zinavyoonekana pichani
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinaelezwa kuwa na wafuasi wengi katika Mkoa wa Arusha na maeneo ya jirani kiasi cha kupelekea tafsiri kuwa eneo hilo ndio ngome yake zaidi hasa kwa kipindi cha sasa katika siasa za ushindani nchini.
Kwa mgeni anaetembelea Jiji la Arusha kwa mara ya kwanza ni wazi atakutana na watu wa jinsia na rika tofauti wakiwa wamevalia mavazi ama kuvipamba na vitambaa au kitu chochote chenye rangi nne za chama hicho.
Hali hii inaonekana kama utamaduni sasa maana haya hufanyika muda wote na sio wakati wa kampeni pekee. Kuna baadhi wenye magari na pikipiki nao wanayaremba kwa chochote chenye rangi za CHADEMA.
Jambo hili lililzaimu Blog hii kufanya uchunguzi mdogo na kugundua kuwapo kwa wajasiriamali wengi ambao wameamua kujiajiri kutengeneza bidhaa za aina mbalimbali zilizopambwa kwa rangi za bendera ya CHADEMA na kuziuza ili kuendesha maisha yao.
Bidhaa hizo ni pamoja na T-Shirts, Skafu, Kofia, Sweta, Stika za magari, Bangili, Hereni, Mikufu, na vifutia jasho kwa wachezaji kwa kuvaa mkononi ama kichwani.
Baadhi yao wamekiri kunufaika na kukubalika kwa chama hicho kwa watu wengi mjini hapa jambo ambalo linafanya wepesi kwa wao wajasiriamali kujipatia kipato kinachowasaidia kuendesha maisha na wengine wakadai wanfanya kama sehemu ya kukitangaza zaidi chama hicho.
Hizi ni bidhaa mabazo tayari zimekamilika kwa ajili ya kuuzia wateja. Bei ni kuanzia Sh 500 hadi 15,000 kwa bidhaa moja
Hapa ni kwa vijana wanaotengeneza bidhaa za urembo wa asili jirani Arusha City Park. Nao wameamua kutumia fursa iliyopo kujiongezea kipato
Kamera yetu iliwansa vijana hawa wakikatiza mitaa ya Jiji na bidhaa zao kutafuta wateja.
Huyu ni mjasiriamali mwingine anaenufaika na umaarufu wa CHADEMA mjini Arusha. Ofisi yake, japo sio rasmi sana ipo jirani na Msikiti wa Ijumaa mjini hapa.
Kamera yetu pia ilimnasa kijana huyu akiwa na begi limejaa t-shirts akitafuta wateja mitaa ya Jiji. Mfano wa sampuli alizo nazo ni kama hiyo aliyoivaa
0 maoni:
Post a Comment