Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mkutano wa Mbunge Msigwa (CHADEMA) wavamiwa, makada wa CHADEMA wacharangwa mapanga na kukimbizwa hospitali

IMG_2993

Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA) Mh Peter Msigwa akiwahutubia wananchi Kijiji cha Nduli kilichopo Manispaa ya Iringa jana

IMG_3002

Hapa Masigwa anamtambulisha aliekuwa Mwenyekiti wa CCM katika eneo hilo alieamua kujiungana CHADEMA sambamba na wanachama wengine zaidi ya 100 wakimfuata.

IMG_2109

Sehemu ya wananchi waliohudhuria mkutano huo wakifurahia kadi za CHADEMA

13052012061

Wakati mkutano ukielekea kumalizika, vijana wanao daiwa kuwa ni watoto wa Diwani wa eneo lile walivamia mkutano nakuanzisha vurugu wakitaka kumvamia Mh. Msigwa na kumdhuru. Vurugu iliyo ilipelekea kukatwa mapanga kwa vijanawa wili wa CHADEMA (pichani), mmoja kukatwa mkono na mwingine kujeruhiwa vibaya usoni kwa mapanga.

13052012062 

13052012063

Kijana wa CHADEMA alie katwa mkono na vijana wa CCM ambao wanasemekana kuwa ni watoto wa Diwani (CCM) wa eneo hilo.

Vijana hao walio leta vurugu katika mkutano kwa sasa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi.

Leo, Mh. Msigwa anatarajia kuongea na vyombo vya habari kuhusu yalio tokea kwenye mkutano wake.

Tukio hili linakuja ikiwa ni takribani wiki moja tangia Kiongozi wa Itikadi na Uenezi (NEC) ya CCM kukansha tuhuma zilizotolewa na viongozi wa CHADEMA wakihusiha matukio ya kuuwawa na kujeruhiwa kwa viongozi na makada wa chama hicho kuwa zinafanywa na CCM kwa lengo la kurudisha nyuma jitihada zao.

Pia, tukio hili linatokea kukiwa na kumbukumbu ya wabunge wengine wawili wa chama hicho kuchaarangwa mapanga na watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa CCM, mbele ya Polisi Kirumba Mwanza mapema mwezi Aprili, 2012. Halkadhalika watu wengine 5 walicharangwa mapanga Kiwira Mbeya siku moja na wabunge hao ambao walihamishiwa Mhimbili kwa matibabu zaidi.

Watu wa CHADEMA pia watapokea taarifa hizi ikiwa ni siku chache zimepita tangia wapokee taarifa nyingine ya kuuwawa kwa kuchinjwa shingi kikatili kwa Mwenyekiti wa chama hicho Kata ya Usa-River, Arusha.

Chanzo: http://mbungeiringamjini.blogspot.com (maelezo ya ziada na blog hii)

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO