Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mwendesha kesi za EPA afariki dunia

MKURUGENZI Msaidizi wa Mashitaka nchini na Mwendesha Mashitaka mashuhuri katika kesi kubwa mbalimbali nchini, Stanslaus Boniface amefariki ghafla.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana jana mchana na kuthibitishwa na Mkurugenzi wa
Mashitaka (DPP), Eliezer Feleshi, Boniface alifariki ghafla jana asubuhi na chanzo cha kifo chake hakijafahamika.

“Boniface amefariki leo (jana) alfajiri katika Hospitali ya Regency alikopelekwa baada ya kujisikia vibaya akiwa nyumbani kwake…msiba upo nyumbani kwake eneo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,” alisema Ofisa Habari wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu (AG), Siatu Msuya.

Boniface alipata umaarufu katika kesi alizokuwa akiziendesha ambazo ni za wizi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu (BoT) ikiwamo inayomkabili kada wa CCM, Rajab Shaban Maranda na wafanyakazi wanne wa BoT wanaodaiwa kuiba Sh 207,284,390.44.

Nyingine ni ile ya wizi wa Sh bilioni 1.1 inayomkabili Bahati Mahenge na wenzake wanne.
Boniface alizaliwa Februari 21, 1968 na ameacha mke na watoto watatu. Amewahi kufanya kazi kama Mwendesha Mashitaka Mkuu katika mikoa ya Mwanza, Mbeya na Dar es Salaam.

Chanzo: HabariLeo

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO