Na Geofrey Nyang’oro
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe juzi usiku alikesha na abiria zaidi ya 1,000 waliokwama kwa saa 11 katika stesheni ya Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (Tazara) jijini Dar es Salaam kutokana treni kukosa mafuta.
Kutokana na tatizo hilo, Dk Mwakyembe ambaye alifika katika stesheni hiyo mara baada ya kuwasili kutoka safarini India, aliahidi kuwashughulikia watendaji wa Tazara waliosababisha uzembe huo.
Dk Mwakyembe ambaye ametimiza siku 20 tangu alipoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuongoza Wizara ya Uchukuzi, alifika eneo hilo baada ya abiria wawili kumpigia simu na kuomba aingilie kati tatizo hilo.
Alifika stesheni katika hiyo saa 4:01 usiku na kukaa mpaka saa 6:30 usiku alipoondoka na hakukuwa na kiongozi yeyote wa ngazi za juu wa Tazara aliyefika kushughulikia tatizo hilo.
Akutana na abiria Baada ya Dk Mwakyembe kuwasili na kuingia katika ukumbi wa kupumuzika abiria wanaposubiri kuondoa, wasafiri walimshangilia kwa nguvu mara baada ya kujitambulisha kuwa ni Waziri wa Uchukuzi na amefika kutatua tatizo linalowakabili, ingawa ni usiku akiwa ametoka safarini India.
Soma zaidi Mwananchi Jumapili, Mei 27, 2012
0 maoni:
Post a Comment