Watu milioni 53 wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaishi chini ya mstari wa umaskini, hivyo juhudi za pamoja zinahitajika ili kuinua maisha yao.
Akiwasilisha matokeo ya ripoti ya 'Hali ya Afrika Mashariki 2012' iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Mradi wa taasisi ya Kimataifa ya Society for International Development (SID) Aidan Eyakuze, alisema asilimia 38 ya wananchi wa EAC ni maskini sana na kwamba nchini Tanzania idadi hiyo imeongeza kwa milioni 4.9 hadi kufikia milioni 14.9 kutoka milioni 10 katika kipindi cha 17.
Eyakuze alisema pamoja na ongezeko hilo kwa Tanzania, Kenya inaonekana kuwa na maskini wengi zaidi kwa kuwa na maskini milioni 18.9, Uganda (milioni 8.3) Burundi (milioni 6.3) na Rwanda (milioni 4.7).
"Chakula cha uhakika bado ni tatizo kubwa lakini jambo la kushangaza ni kwamba tuna ardhi nzuri na tunatumia mbolea kwenye kilimo chetu, swali linabakia ni kwa nini tuna njaa, kwa nini hatuwezi kulisha watu wetu?" alihoji.
Chanzo: Nipashe, Mei 25, 2012
0 maoni:
Post a Comment