WAFANYABIASHARA wa ndani na nje ya nchi wametakiwa kutumia fursa za kibiashara wakati wa mkutano wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) utakaohusisha Marais kutoka katika nchi mbali mbali za Afrika unaotarajia kufanyika Mei 28 hadi Juni 2 Mkoani Arusha.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo wakati aliipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya mkutano huo mkubwa unaotarajia kujumuisha watu 2500 hadi 3000 kutoka nchi mbalimbali.
Alisema wafanyabiashara hawana budi kubuni biashara ambazo zitaingiza kipato katika mkutano wa benki ya maendeleo ya Afrika (AfDB) pia aliwaasa wamiliki wa hoteli pamoja na watoa huduma za utalii kutoa lugha nzuri kwa wageni hao ambao wanakuja kwaajili ya mkutano huo na wengine kutembelea mbuga za wanyama zilizopo Tanzania.
Alisema ni vema wamiliki wa oteli kuwakumbusha wafanyakazi wao kutoa lugha nzuri kwa wageni mbalimbali wanaokuja Tanzania hususan Arusha kwaajili ya utalii na shughuli mbalimbali pia wale wanaotoa huduma za utalii nao watoe huduma nzuri ili waweze kupata watalii wengi nchini.
“Mkutano huu ni fursa kwa wafanyabiashara,watu wa utalii na nk kujiingizia vipato hivyo tumieni lugha nzuri ili hawa watu waweze kuja zaidi na kuleta maendeleoa kkatika nchi yetu”.
Naye Mkurugenzi wa Kituo cha Mikutano cha IACC, elishilia Kaaya alisema AICC imejipanga vyema kwaajili ya mkutano na kuwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo ya kibiashara.
Alisema kinachofanyika hivi sasa ni kuangalia namna gani watatumia fursa hiyo kwa ajili ya kuhakikisha wageni watanufaika na mkutano huo ambapo jumla ya mgavana 80 watashiriki pamoja na marais 10 toka nchi mbali mbali
Aliongeza kuwa hivi sasa tayari maandalizi mbali mbali yameanza kufanyika ilimradi kuhakikisha kuwa mkoa wa ARUSHA utananufaika na mkutano huo wa uwekezaji lengo likiwa nikuongeza pato la taifa kiuchumi.
CHANZO: Mtandao wa Dullonet
0 maoni:
Post a Comment