Mh Godbless Lema akigawa kadi za CHAEMA kwa kina mama aliojitolea kuwalipia mkutanoni viwanja vya Kwasakwasa, Same Mjini jana.
Mamia ya wananchama wapya waliandikshwa na kupatiwa kadi za uanachama.
***
Aliekuwa Mbunge wa Arusha Mjini ambae kwasasa anasubiria hukumu ya rufaa ya kupinga kuvuliwa ubunge wake, Mh Godbless Lema amewaasa watanzania kutokubali kurubuniwa na wanasiasa wanaotaka kuwagawa kwa misingi ya ubaguzi wa kidini, kikabila au eneo watokako ili waweze kuwatawala kwa uraisi.
Mh Lema ameyasema hayo jana jioni katika mkutano wa hadhara wa CHADEMA uliofanyika katika viwanja vya Kwasakwasa, Same Mjini ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara ya kichama kwa siku nne Wilayani humo.
Alisema kwamba kwa muda mrefu kumekuwepo na matamshi ya viongozi mbalimbali yanayoashiria kuwagawa watanzania katika misingi ya ubaguzi, mfumo ambao alidai umetokana na mbinu ya wakoloni aliyoiita “divide and rule” au “wagawe uwatawale'” kwa Kiswahili.
Mbali na hilo, Mh Lema pia alimtaka Rais Kikwete kuwashughulikia wezi wote wa mali ya umma na kudai kwamba kama ataonekana kuendelea kuachia watu hao wanazidi kuliibia taifa basi atatolewa madarakani kwa mujibu wa sheria.
Akisisitiza zaidi, Lema alisema kuwa watanzania “wamesaini mkataba” na Serikali ya Kiwete kuwapatia maisha bora na si vinginevyo.
Akihutubia mamia ya watu waliofurika viwanja hivyo huku wakimshangilia, Mh Lema alikumbushia siku 14 alizodai kukaa gerezani Kisongo kwa hiari yake ambako alidai kujifunza mambo mengi na kugundua jinsi watu wanavyonyimwa haki zao.
Alitolea mifano ya watu aliowakuta wakitumikia vifungu ambavyo walimwambia havikuwastahili na wengine kesi zao hazisomwi na kujikuta wakiishi gerezani kwa zaidi ya miaka 9 bila hatia.
Alisema moja kati ya matukio yaliyomsikitisha ni la kijana mmoja aliemueleza kuwa amefungwa maisha kwa uonevu baada ya kutengenezewa kesi ya ubakaji kwasababu tu alikuwa na mahusiano na mtoto wa Waziri mmoja nchini (jina linahifadhiwa)
Lema alisema pia alikutana na mzee wa miaka 85 ambae ane amefungwa maisha kwa makosa ya kubaka lakini akadai kuwa mze huyo anasema alitengenezewa kesi hiyo ili watu waliomshitaki waweze kuuza shamba lake, na kwamba akiwa gerezani walimpelekea mikataba asaini.
Katika mkutano huo, walikuwepo pia viongozi wengine na makada wa chama hicho ambao walihutubia pia, akiwemo Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, Mh John Heche, Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Kilimanjaro, Mh Augustino Matemu maarufu kama Papaa Makelele.
Wengine ni aliekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Arusha, James Ole Millya na kada mwenzake ambae nae alikuwa mjumbe wa NEC, Ngd Ally Bananga, aliekuwa Diwani wa Sombetini (CCM), Alphonce Mawazo na Wilson Matata ambae ni Mwenyekiti wa vijana CHADEMA Babati.
0 maoni:
Post a Comment