Mh Godbless Lema akiongozana na Kamanda mpya wa chama chake, Ally Bananga ambae aliwahi kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mahusiano Arusha, wakiwasili viwanja vya NMC Jijini Arusha leo
Wazee wa kimila (Masai, waliovalia mgolole) Wazee hawa ndio walimpa James Ole Millya kiapo cha kimila na kumsihi kutokuwa kigeugeu kama kinyongaMwenyekiti wa CHADEMA, Mh Mbowe akihutubia mkutanoni hapo ambapo ameeleza kuwepo kwa wabunge 70 miongozi mwa wabunge zaidi ya 200 wa CCM ambao wamemtaarifu nia yao ya kujiunga na CHADEMA. Akasema pia wapo Mawaziri 9 katika Baraza hili jipya alilotangaza Rais Kikwete jana, kuwa nao wamemtaarifu nia yao hiyo.
Baadae Mbowe akaelezea namna Kikwete alivyokiuka Katiba ya nchi mara mbili katika uteuzi wake wa Mawaziri jana jambo ambalo amedai wataliwasilisha Bungeni mwezi wa sita.
Aliekuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Themi (wapili toka kushoto) na aliekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Arusha akihughulikia Mahusiano, Ally Bananga (watatu toka kushoto) wakiongozwa na Mh Lema kwenda kutupa kadi zao za CCM walizorudisha kwenye pipa maalumu viwanjani hapo, halionekani pichani
Wazee wa kimila wakiomuapisha James Ole Millya kiapo cha kimila na kumtaka kutokiuka kiapo hicho na kwamba endapo atakiuka basi wao wasilaumiwe kwa yatakayotokea
Wananchama wapya kutoka Monduli wakiingia viwanjani hapo kwa mabango yenye jummbe mabalimbali kwa Serikali na Chama Cha Mapinduzi walichokihama
Maefu ya wafuasi wa CHADEMA waliohudhuria mkutano huo wakiitikia salamu ya “Peoples-Power” kwa ishara ya ngumi kama walivyokuwa wakiongozwa na Mh Mbowe (hayupo pichani)
Hapa ni baadhi ya kadi za CCM zilizorudishwa zikidondoshwa toka juu jukwaani kuangua kia kwenye pipa maalumu chini
Ole Millya akikaribishwa rasmi na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe. Pichani Mbowe akijiandaa kumvisha skafu ya cha kipya
0 maoni:
Post a Comment