Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Breaking News: Rais Kikwete atangaza mawaziri wapya jioni hii; Ngeleja, Nundu, Maige, Mponda, Mkulo waachwa

Kitendawili cha nani kuachwa au kuendelea kwenye usukaji upya wa Baraza la Mawaziri kimeteguliwa jioni hii baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutangaza orodha ya wateule wake wapya Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mawaziri wengi wemeendelea kuwemo katika Baraza la awali huku baadhi wakihamishiwa wizara nyingine.

Baadhi ya mawaziri walioachwa katika uteuzi wa Rais ni pamoja na William Ngeleja, Omar Nundu, Mustafa Mkulo, na Ezekie Maige, Haji Mponda.

Akitangaza Baraza lake hilo, Rais Kikwete amesema muundo wa Baraza haujabadilika.

Ameeleza kuwa kila aliesababisha Waziri kubeba dhamana ya kuwajibika kisiasa kwa makosa ya waliochini yake, nae hataachwa.

viewer

ORODHA YA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI

MAWAZIRI

1. OFISI YA RAIS

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu)

Ndugu Stephen M. Wasira, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora)

Ndugu George Mkuchika, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (UTUMISHI)

Ndugu Celina Kombani, Mb.,

2.      OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO)

Ndugu Samia H.  Suluhu, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA)

Dr. Terezya P.L. Huvisa, Mb.,

3.      OFISI  YA WAZIRI MKUU

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji)

Ndugu Mary M. Nagu, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)

Ndugu Hawa Ghasia, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge)

Ndugu William V. Lukuvi, Mb.,

4.      WIZARA

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Ndugu Samuel J. Sitta, Mb.,

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Mb.,

Waziri wa Ujenzi

Dr.  John P. Magufuli, Mb.,

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii

Dr. Hussein A.H. Mwinyi, Mb.,

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi

Dr. Shukuru J. Kawambwa, Mb.,

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto

Ndugu Sophia M. Simba, Mb.,

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Ndugu Bernard K. Membe, Mb.,

Waziri wa Katiba na Sheria

Ndugu Mathias M. Chikawe, Mb.,

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

Ndugu Emmanuel Nchimbi, Mb.,

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi

Dr. David M. David, Mb.,

Waziri wa Kazi na Ajira

Ndugu Gaudentia M. Kabaka, Mb.,

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia

Prof.  Makame M. Mbarawa, Mb.,

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Prof.  Anna K. Tibaijuka, Mb.,

Waziri wa Maji

Prof. Jumanne Maghembe, Mb.,

Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum

Prof. Mark Mwandosya, Mb.,

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika

Eng. Christopher Chiza, Mb.,

Waziri wa Uchukuzi

Dr. Harrison Mwakyembe, Mb.,

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

Dr. Fenella E. Mukangara, Mb.,

Waziri wa Maliasili na Utalii

Ndugu Khamis Kagasheki, Mb.,

Waziri wa Viwanda na Biashara

Dr. Abdallah O. Kigoda, Mb.,

Waziri wa Fedha

Dr. William Mgimwa, Mb.,

Waziri wa Nishati na Madini

Prof. Sospeter Muhongo, Mb.,

5.      NAIBU MAWAZIRI

OFISI YA RAIS

HAKUNA NAIBU WAZIRI

6.      OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais

Ndugu Charles Kitwanga, Mb.,

7.      OFISI YA WAZIRI MKUU

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)

Ndugu Majaliwa K. Majaliwa, Mb.,

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)

Ndugu Aggrey Mwanry, Mb.,

8.      WIZARA MBALIMBALI

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira

Dr. Makongoro M. Mahanga, Mb.,

Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika

Ndugu Adam Malima, Mb.,

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

Ndugu Pereira A. Silima, Mb.,

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara

Ndugu Gregory G. Teu, Mb.,

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi

Ndugu Benedict N. Ole-Nangoro, Mb.,

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Ndugu Mahadhi J. Maalim, Mb.,

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo  ya Makazi,

Ndugu Goodluck J. Ole-Medeye, Mb.,

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto

Ndugu Ummy A. Mwalimu, Mb.,

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi

Ndugu Philipo A. Mulugo, Mb.,

Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Dr. Abdulla Juma Abdulla, Mb.,

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii

Ndugu Lazaro Nyalandu, Mb.,

Naibu Waziri wa Ujenzi

Ndugu Gerson Lwenge, Mb.,

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,

Dr. Seif Suleiman Rashid, Mb.,

Naibu Waziri wa Nishati na Madini

Ndugu George Simbachawene, Mb.,

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia

Ndugu January Makamba, Mb.,

Naibu Waziri wa Uchukuzi

Dr. Charles J. Tizeba, Mb.,

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

Ndugu Amos Makala, Mb.,

Naibu Waziri wa Maji

Eng. Dr. Binilith Mahenge, Mb.,

Naibu Waziri Nishati na Madini

Ndugu Stephen Maselle, Mb.,

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria

Ndugu Angela Jasmine Kairuki, Mb.,

Naibu Waziri wa Fedha

Ndugu Janet Mbene, Mb.,

Naibu Waziri wa Fedha

Ndugu Saada Mkuya Salum, Mb.,

Wataapishwa Jumatatu tarehe 8 Mei, 2012 saa 5.00 asubuhi katika viwanja vya Ikulu

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

Dar es Salaam.

4 Mei, 2012

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO