Taarifa za hivi punde zilizotufikia kutoka vyanzo vya kuaminika zinaeleza kuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Mh Joshua Nassari amejisalimisha Polisi Makao Makuu Arusha kama alivyohitajika kwa mujibu wa maagizo ya Naibu Kamishina wa Jeshi la Polisi nchini, Isaya Mngulu aliesema Polisi inamtaka Mbunge huyo ajisalimishe kabla ya saa 12 jioni (juzi).
Inaelezwa kuwa Nassari alifika ofisini hapo majira ya saa sita mchana huu na kupokelewa na askari wa kawaida waliomweleza kuwa viongozi wao wapo kwenye kikao muda huo.
Taarifa hizo zinafafanua zaidi kwamba baada ya kitambo kidogo kupita, Mh Nassari aliamua kuondoka na kurejea Jimboni kwake kwenda kuendelea na mkutano na wananchi.
Katika kujisalimisha kwake, Nassari alikuwa ameambatana na aliekuwa Mbunge wa Arusha Mjini akisubiri rufaa ya kupinga kuenguliwa kwa ubunge wake, Mh Godbless Lema, na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) Mh John Heche.
Weingine ni Ngd Ally Bananga aliewahi kuwa kiongozi wa UVCCM Arusha kabla ya kujiunga kwake na CHADEMA na viongozi wengine wa chama, pamoja na waandishi wa habari.
Hitaji la kujisalimisha kwa Mh Nassari kunatokana na kile kilichoelezwa na Mngulu kuwa ni kutokana na maneno waliyotoa katika mkutano wa hadhara Jumamosi ambayo yanadaiwa kuwa ya uchochezi ingawa hayakutajwa ni maneno gani.
0 maoni:
Post a Comment