Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Hatma ya Ubunge wa Mnyika kujulikana Mei 24

Mnyika-1 HUKUMU ya kupinga matokeo ya ubunge katika jimbo la Ubungo iliyofunguliwa na mgombea wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Hawa Ng’umbi dhidi ya mbunge wa jimbo hilo John Mnyika itatolewa Mei 24, mwaka huu.

Jaji Upendo Msuya wa Mahakama ya Kazi alieleza hayo baada ya kusikiliza majumuisho ya pande zote mbili.

Awali katika majumuisho hayo Wakili Mkuu wa Serikali, Justus Mulokozi, anayemtetea Mwanasheria Mkuu wa Serikali alidai kuwa hakukuwa na ushahidi wa kuthibitisha madai yote yaliyotolewa na mlalamikaji ikiwemo ya kuzidi kwa kura ambapo alidai mdai hajui ziliathiri uchaguzi mkuu na hakuna shahidi mwingine aliyejitokeza kuhusiana na hilo.

Alisema madai ya udhalilishwaji na kuitwa fisadi, Wakili Mulokozi alidai kuwa shahidi wa pili katika kesi hiyo Robert Kondela hakusema kauli hiyo iliathiri uchaguzi na mleta madai alishawahi kuhojiwa katika runinga kuhusiana na tuhuma hizo hivyo suala hilo alikujitokeza wakati wa kampeni bali lilishakuwepo hivyo anatakiwa kuwashtaki walioanzisha.

Naye wakili Edson Mbogoro anayemtetea Mnyika alidai kuwa si kila aina ya dosari inayojitokeza katika uchaguzi lazima iathiri akielezea hoja iliyotolewa na mlalamikaji ya maneno ya kashfa Septemba 11, 2010 lakini cha kushangaza alitegemea shahidi wa pili ambaye naye alishindwa kuthibitisha hilo kwa sababu siku iliyotajwa hakukuwa na mkutano uliofanyika.

Mbogoro pia alidai kuwa shahidi huyo alidai kuwa Mnyika alikuwa akitangaza nia ya kugombea ubunge kitu ambacho si kawaida kwani kampeni zilikwishaanza.

Wakili huyo aliiomba mahakama kutupia mbali madai yote matano ikiwemo na upande wa madai kulipa gharama zote za uendeshaji kesi.

Wakili Maige aliiomba mahakama hiyo ibatilishe matokeo ikiwemo upande wa wadaiwa kulipa gharama zote za kesi namba 107/2010, Ng’humbi anaiomba mahakama hiyo ibatilishe matokeo yaliyompa ushindi Mnyika.

Alidai Mnyika akiwa na wafuasi wengine wa CHADEMA wakiwa katika ofisi za msimamizi wa uchaguzi walimtishia na kumshinikiza ahakikishe kuwa wanashinda.

Anadai pia kuwa wakati wa kujumlisha matokeo msimamizi wa uchaguzi alitumia kompyuta ndogo (laptop) ya Mnyika badala ya ile ya tume tena bila kuikagua kuona kama kulikuwa na taarifa za kupikwa.

Anaongeza kuwa katika fomu nyingine za matokeo mawakala wa Mnyika walighushi saini za mawakala wa vyama vingine na kwamba katika vituo vingine wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi hawakuwasilisha fomu namba 21B za matokeo.

Katika hatua nyingine Fred Mpendazoe kupitia Wakili wake Peter Kibatala amepanga kuwasilisha hoja ya kukata rufaa ya hukumu iliyotolewa na Jaji Ibrahim Juma Mei 2, mwaka huu, iliyohalalisha ubunge wa Dk. Makongoro Mahanga (CCM) katika jimbo la Segerea kuwa mbunge.

Chanzo: Tanzania Daima

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO