Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

John Mnyika Ashinda Kesi Ya Kupinga Ubunge Wake

2 (7) Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika ameshinda kesi ya kupinga ushindi wake katika Jimbo la Ubungo katika uchaguzi wa mwaka 2010, hukumu iliyotolewa leo na Mahakama Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam. Pichani wafuasi wa Chadema wakiwa wamembeba juu kwa juu mara baada ya kutangazwa mshindi. (Maelezo na Picha: Daily Mitkas Blog)

Hawa

Mama Hawa Ngh’umbi (mwenye suti ya kijivu) akisalimiana na watu wake mara baada ya Mahakama kutupilia mbali pingamizi zake dhibi ya ushindi wa John Mnyika!!

**********

MBUNGE wa jimbo la Ubungo John mnyika ameibuka kidedea katika kesi iliyofunguliwa dhidi ya Ubunge wake na aliekuwa mpinzani wake kwenye Uchaguzi Mkuua wa 2010, Hawa Ng'humbi.

Kesi hiyo iliyovuta hisia za watu wengi, imehitimishwa na uamuzi wa Jaji wa Mahakama Kuu aliekuwa anasikiliza shauri hilo kwa kutupilia mbali mashitaka yote dhidi ya mbunge huyo, ambayo ni...
1)Kwamba Mnyika alimtuhumu kuuza nyumba za UWT
2)Kutumia Laptop za Mnyika Kuhesabu kura
3)Kuingia watu wengi wa CHADEMA katika chumba cha kuhesabia kura
4)Kuzidi kwa kura hewa 16,000
5)Kukosewa kwa karatasi za kujumulisha kura (form)na kutaka mshitaki kulipa gharama zote za kesi hio. Na mshitaki Bi. Hawa kutakiwa kulipa gharama zote za kesi hio.

mnyika

Mh John Mnyika (mwenye kombati) akifurahia na watu wake. Picha na Kili News Blog

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO