Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Lema awaasa vijana kupunguza starehe ili kupata fedha za kuchangia mabadiliko nchini

DSCN3048

Mh Godbless Lema (mwenye kofia) akifuatilia kwa makini hotuba ya Alphonce Mawazo (haonekani pichani), aliekuwa Diwani wa Sombetini (CCM) akizungumza na wanachuo wa Cho cha Uhasibu Arusha jana, ambao ni wanachama na wapenzi wa CHADEMA. Wengine katika picha ni viongozi na makada wa chama hicho Mkoani Arusha.

*******************

ALIEKUWA Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema ambae anasubiri hukumu yarufaa yake aliyoiwasilisha Mahakama ya Rufaa takribani wiki mbili zilizopita akipinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kumvua ubunge wake, amewaasa vijana nchini kuanza tabia ya kunguza bajeti ya matumizi yasiyi ya lazima ili waweze kupata kiasi kidogo cha fedha ambacho wataweza kuchangia harakati wanazoshiriki kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini yanayopiganiwa na chama chake.

Mh Lema alitoa rai hiyo wakati alipokuwa akijibu risala ya wanachuo wa Chuo cha Uhasibu Arusha (AIA), wanachuo ambao ni wanachama, wapenzi na wafasi wa CHADEMA tawi la chuo hicho katika hafla iliyofanyika Kisaki Villa Inn iliyopo Njiro kuwaaga wenzao wanaomaliza masomo.

Awali, wanachuo hao makamanda wa CHADEMA walimweleza mgeni rasmi (Mh Lema) kuwa wanakabiliwa na hitaji la shilingi mil 1,000,000 kwa ajili ya shughuli za uboreshaji tawi la chama chuoni hapo.

Mh Lema aliwambia endapo watapunguza safari za kwenda disco, vilabuni na maeneo mengine ya starehe, wanaweza kubaki na salio ambalo litawawezesha kutimiza malengo yao bila kuomba omba misaada ya mahitaji ambayo yako nadani ya uwezo wao.

Katika hafla hiyo, walikuwepo pia makamanda wengine wa chama hicho ambao nao walipata fursa ya kuzungumza na wanachuo hao.

Walikuwepo Ndg James Ole Millya, Ally Bananga na Alphonce Mawazo ambao wamejiengu a CCM hivi karibuni na kujiunga na CHADEMA.

Wengine ni Mwenyekiti wa Vijana CHADEMA Wilaya ya Hai, Mss Doris Cornelly, Madiwani wa chama hicho Arusha, Mwenyekiti wa Vijana CHADEMA Arusha Mh Ephata Nanyaro pamoja na Katibu wake ambae pia ni kiongozi wa Tawi la chama hicho Arusha University, Julisiza Mengiseni.

Hafla hiyo ilihitimishwa na zoezi la kuchangisha fedha, zoezi lililoendeshwa na kusimamiwa na Mh Lema ili kupata fedha ambazo wanafunzi hao walikuwa wanazihitaji kwa shughuli za tawi lao.

DSCN3041 Alphonce Mawazo, aliekuwa Diwani wa Sombetini (CCM) kabla ya kuhamia CHADEMA, akizungumza na wanachama wa CHADEMA Tawi la Uhasibu jana

DSCN3073James Ole Millya nae alikuwepo kuwapa neno vijana hao wasomi

DSCN3087 

Mh Lema akipokea risala ya wanachama (CHADEMA) hao tawi la chuo cha Uhasibu Arusha

DSCN3119

Mh Lema akishiriki kuhesbau fedha zilizochangwa katika hafla hiyo. kshoto kwake ni Diwani wa Revolosi (CHADEMA) Mh Ephata Nanyaro akirudisha chenji kwa mmoja wa wachangiaji

DSCN3125

Ally Bananga (anepiga makofi) akifurahia jambo na waalikwa wengine katika hafla hiyo. Ally alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu CCM (Vijana) kabla ya kujitoa CCM na kujiunga na CHADEMA wiki chache zilizopita ambapo amekuwa akishiriki mikutano mabalimbali ya kimarisha chama chake kipya ka kuanza na mkutano wa kutambulishwa kwake na James Millya mwezi uliopita  viwanja vya NMC Jijini Arusha. Baadae alisafiri hadi Same kuungana na John Heche kwenye ziara ya siku nne Wilayani humo. Alipomaliza hapo alishiriki Mkutano wa Kata ya Olasiti, mkutano ambao ulihudhuriwa pia na Lema. Leo anatarajiwa kuungana na makamnada wengine wa chama hicho kufanya ziara ya kuimarisha chama Wilayani Mwanga akiungana na Kiongozi wa CHADEMAWilaya ya Kinondoni Dar es Slaam, Ndg Henry Kileo.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO