Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

BAVICHA Arusha waunga mkono tamko la Mwenyekiti wao

BARAZA la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Arusha limeunga mkono tamko lililotolewa na mwenyekiti wao wa taifa, John Heche, dhidi ya Mbunge wa Maswa Mashariki, John Shibuda, na kukiomba chama hicho kuchukua maamuzi magumu ya kumtimua mbunge huyo.

Mwenyekiti wa BAVICHA mkoani hapa, Ephata Nanyaro, aliyasema hayo jana alipoongea na waandishi wa habari, na kudai kwamba vijana wamesikitishwa na kauli ya kukidhalilisha chama chao iliyotolewa na Shibuda kwenye mkutano wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Alisema kuwa wao hawana tatizo na nia yake ya kugombea urais mwaka 2015 bali wamefadhaishwa na madai kuwa chama pekee kinachoweza kushika dola ni CCM jambo walilosema ni sawa na uhaini.

Tayari Vijana wa mikoa ya Shinyanga na Pwani nao wametoa tamko lao kumunga mkono Mwenyekiti wao taifa.

DSCN3130Mwenyekiti wa BAVICHA Arusha (katikati) akiwa na baabdhi ya vijana wa chama hicho Jijini Arusha jana 

**********

TAARIFA KWA UMMA
BAVICHA mkoa wa Arusha,inaunga mkono Tamko la BAVICHA Taifa, juu ya hatua ya Mh Shibuda kutoa Tamko la kukidhalilisha chama mbele ya viongozi wa ccm. Kimsingi BAVICHA hatuna tatizo na nia ya Mh Shibuda kugombea urais, bali kauli yake kuwa chama pekee kinachoweza kushika dola ni ccm.

BAVICHA tunalaani kauli hii, na tunapenda kuujulisha umma wa Tanzania kuwa CHADEMA imejipanga kuchukua Dola, ina mfumo mzuri wa kiuongozi kutoka chini, hadi Taifa. Ni chama pekee chenye Katiba bora na kinachotetea kwa vitendo masilahi ya umma, ni tumaini pekee kwa mamilioni ya Watanzania.

Kimsingi Mh Shibuda anaweza kuwa anatumiwa na ccm kuvuruga FOCUS yetu, kutokana na operesheni Vua Gamba Vaa Gwanda ambayo imekuwa na mafanikio makubwa sana, ambapo maelfu ya viongozi wa ccm wanahamia CHADEMA, huu ni mkakati wa ccm kumtumia Shibuda. Tunawaambia kuwa kamwe hatutapoteza Focus yetu,na tumeshtukia mpango huu mapema,tunasonga mbele hadi kieleweke.

Chama chetu kimepita katika mapambano na changamoto mbalimbali. Ni chama pekee ambacho kimewahi kuchukua maamuzi magumu na kubaki imara. Katika hili la Mh Shibuda tunaomba chama kichukue maamuzi magumu, hata kwa gharama ya Jimbo.

Ukiwa na askari katika kikosi chako ambaye anaamini majeshi ya adui ni bora zaidi na yanastahili kushinda vita askari huyo anakuwa ni msaliti na anapofanya kazi au jitihada ya kutaka adui ashinde kijeshi huo ni uhaini. Shibuda kutangaza kuwa anataka kugombea Urais kupitia CHADEMA mwaka 2015 siyo tatizo.Tatizo ni kukidhalilisha chama mbele ya CCM.

Imetolewa na
Nanyaro E.J
Mwenyekiti BAVICHA Mkoa Wa Arsha

21 Mei 2012

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO