Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Nassari kushitakiwa kwa uchochezi

MBUNGE wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari na viongozi wengine wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanasubiri kufikishwa mahakamani na Jeshi la Polisi ikiwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) atakubali, kwa kile kilichodaiwa kupatikana na makosa ya uchochezi.

Nassari, Mwenyekiti wa BAVICHA taifa, John Heche na Ally Bananga ambaye amehamia chama hicho Jumamosi akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM) alikokuwa akishika nyadhifa mbalimbali za uongozi, walishikiliwa na kuhojiwa na polisi kwa siku mbili, kabla ya kuachiwa kwa dhamana.

Naibu Kamishina wa Polisi, Isaya Mungulu, aliwaeleza waandishi wa habari jana kuwa baada ya kuwahoji wamebaini makosa wanayowatuhumu nayo yanaangukia katika kifungu cha sheria namba 63 b cha kanuni ya adhabu, sura namba 16, ambapo inahitaji ridhaa ya DPP kabla ya kuyafikisha mahakamani.

Hata hivyo, alisema kuwa hawezi kujua itachukua muda gani kwa DPP kupitia faili hilo na kulirudisha, kwani anashughulika na mafaili mengi,  jambo alilosema kuwa ndilo lililowasababisha kuwaruhusu watuhumiwa hao kuendelea na shughuli zao mpaka watakapowaita.

Wote pamoja na Nassari wanatuhumiwa kuwa kwenye mkutano wao wa Operesheni Vua Gamba Vaa Gwanda walioufanya Jumamosi iliyopita kwenye viwanja vya NMC wanadaiwa kusema kuwa Ridhiwani Kikwete anao marafiki wa kike anaowatambulisha kwa baba yake Rais Jakaya Kikwete, ambaye huwateua kushika nyadhifa mbalimbali kutokana na ushawishi wake.

“Maneno yaliyotamkwa ambayo tunawahoji ni kama kusema endapo Jeshi la Polisi litakuwa halijakamata mtu yeyote kuhusiana na mauaji ya mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Usa River wilayani Arumeru, basi rais asikanyage Arusha na wataweka mipaka mikoa ya Kanda ya Kaskazini na baadhi ya mikoa ya Kanda ya Ziwa, tena mmoja akijitangaza kuwa rais na mwingine kuwa waziri mkuu,” alisema Mngulu alipoongea na waandishi wa habari mwanzoni mwa wiki.

Mngulu alisema kuwa mbunge huyo wa Arumeru Mashariki alikiri kutoa matamshi hayo, ingawa alifafanua kuwa hakuwa na maana hiyo, bali zilikuwa ni kauli za kisiasa tu.

Nassari na Heche waliwaeleza waandishi waliokuwa wamekusanyika eneo la polisi mara baada ya kuachiwa kuwa watatoa kauli mara baada ya kujadiliana na viongozi wao wa chama.


Published bya Tanzania Daima, 10th May, 2012
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO