Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Shibuda amshambulia Mwenyekiti wa BAVICHA kwa maneno makali

Mgogoro baina ya Mbunge wa Maswa Mashariki (CHADEMA) Mh John Shibuda na vijana wa CHADEMA unaonekana kuingia hatua nyingine baada ya mbunge huyo kujibu mapigao kwa mshambulia Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) Ndg John Heche kwa maneno makali na kumuita mkandarasi wa majungu, mnyampala na kawamba ana hila, visa, chuki binafsi dhidi yake yeye Shibuda.

Shibuda alisema maneno hayo wakati alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Power Jam kupitia Capital Redio ya Jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo.

Katika mazungumzo yake, Shibuda aliponda tamko lililotolewa kwenye vyombo vya habari na kiongozi huyo wa vijana CHADEMA Mei 16 mwaka huu kufuatia kauli zake alizotoa kwenye kikao cha NEC ya CCM majuzi, na kudai tamko lile ni mawazo ya mtu mmoja tu kwa chuki zake binafsi.

Katika tamko hilo, BAVICHA walieleza kushtushwa na mambo manne (1)(Shibuda)Kutoa Kauli hiyo kwenye kikao cha NEC ya CCM (2) Kumtangaza meneja wa kampeni zake kuwa ni Mwenyekiti wa CCM Taifa Jakaya Kikwete (3) Kusema kuwa hakuna chama kingine chenye uwezo wa kuiongoza nchi kwa sasa, na (4) Kutoa tamko hilo kwa niaba ya APRM (Mpango wa Kutahmini Utawala Bora Afrika), mambo ambayo walidai ndio yaliwashtua na kuwafedhehesha sana kama vijana hao wa CHADEMA na ndio maana wakalazimika kutoa kauli kuhusiana na suala hilo,

Moja ya mazimio ya tamko hilo lilisema kuwa kwa kitendo cha Shibuda kusema kuwa hakuna chama kingine chenye uwezo wa kuongoza nchi ni kuwadhalilisha vijana wa CHADEMA na watanzania wote ambao leo wanaiona CHADEMA kama tumaini pekee la kuwakomboa, kauli ambayo waliamini kama vijana wa CHADEMA kuwa mamlaka za nidhamu hazitakaa kimya na kuiachia kauli ya namna hii iachwe bila kutakiwa maelezo ya kina. BAVICHA waliahidi kuitisha kikao cha BARAZA na kuijadili kauli hiyo na kuwasilisha mapendekezo yao kwenye vikao halali vya chama.

Aidha, katika hatua yingine Shibuda ameendelea kusimamia msimamo wake kwamba ni kweli alitangazia nia yake hiyo kwenye vikao vya CCM na kwamba amemuomba Kikwete awe meneja wa kampeni zake.

Mtangazaji akauliza kutaka kujua ni kwanini amemtaka Mwenyekiti wa CCM, Mh Jakaya Kiwete kuwa kampeni meneja wake na kama amemkubalia ombi lake hilo. Shibuda  akasema Kikwete  amemuambia kuwa ataangalia muwakilishi aneafaa kwa nchi na kuwa meneja wake.

Akitetea masimamo wake huo, Shibuda alisema sababu hasa iliyomfanya akatangazie kwenye vikao vya CCM na kumpendekeza Mwenyekiti wa chama hicho awe kampeni meneja wake, ni kile anachoamini kuwa kura za wanaCCM zitatokana na mwanaCCM kumwambia kuwa yeye yuko bora.

Akatolea mfano wa mgombea wa CHADEMA kwenye Uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Mh Antony Komu kuwa nae alienda kuomba kura kwa wanaCCM.

“Ukitaka kuoa kwa wasambaa unatafuta mshenga msambaa” alisema Shibuda kamba kawaida ya vibwagizo vyake.

Akihitimisha mahojiano, Shibuda alidai kuwa hajaliona tamko la BAVICHA na kaahidi kuwa atarudi Dar es Salaama na kuitisha mkutano na waandishi wa habari kuelezea sakata hilo ambalo limekuwa gumzo kwa wanachama wa chama hicho ambao wengi wanataka afukuzwe kutokana na tabia zake.

Nae Mwenyekiti wa BAVICHA, John Heche alikiri kusikia maneno hayo kutoka kwa watu tofauti waliompigia simu. Heche amesema kuwa wao (BAVICHA)  kama taasisi ya chama, wanasubiri kwa hamu huo mkutano wa Shibuda na wandishi wa habari, na ndipo watajua hatua inayofuata kwa mujibu wa taratibu za chama.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO