Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mh Freeman Mbowe akihutubia mkutano mkubwa wa uzinduzi wa programu mpya ya chama chake ya Movement for Change (M4C) katika viwanja vya Jangwani Dar es Salaa jana. Alisema harakati za mabadiliko yanayofanywa sasa na chama hicho kupitia kaulimbiu yao ya (M4C) ni maandalizi ya kushika dola mwaka 2015 na kuwataka wananchi kushiriki kwa kila namna katika harakati hizo
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa akihutubia jana Jangwani, alisema taifa lipo katika hali ngumu ikiwamo, mfumuko wa bei, unaosababisha kupanda kwa gharama za maisha kunakochangiwa na na matumizi mabaya ya serikali.
Mbunge wa Singida Mashariki na Mnadhimu wa Kambi ya Upinzania Bungeni, Mh Tindu Lissu akihutubia jana. Aliwataka wananchi kufahamu umuhimu wa Katiba na kuweza kutoa maoni yatakayohitimisha utawala wa kichifu nchini.
Mbunge wa Ubungo, Mh John Mnyika akihutubia wananchi jangwani jana. Mbowe, Dr Slaa na Lissu ndio walikuwa wazungumzaji wakuu wa mkutano huo. (Picha hizi za mwanzo zimepatikana kwa msaada wa Blog ya Kulikoni Ughaibuni)
Sehemu ya umati wa watu waliojitokeza kwenye Mkutno wa CHADEMA katika viwanja vya Jangwani ambapo mamia ya watu walirudisha kadi zao za vyama vya awali nakujiunga na chadema katika muendeleo za programu yao mpya maarufu kama “Vuguvugu la Mabadiliko” – M4C
Baadhi ya kadi za CCM na vyama vingine zilizorudishwa leo na kupatiwa kadi mpya za CHADEMA leo katika mkutano wa M4C Jangwani
Kutoka kushoto, Mh Tundu Lissu, Mh Godbless Lema, Mh Ezekiel Wenje, Mh Joseph Mbilinyi (Sugu)
Sugu, Mbunge wa Mbeya Mjini akighani mbele ya maelfu ya watu waliofurika viwanjani hapo leo
Mbunge wa Kawe (CHADEMA) na Waziri Kivuli wa Ardhi, Mh Halima Mdee akiwasili viwanja vya jangwani leo
Mkurugenzi wa Halamshauri na Bunge CHADEMA, Ndg John Mrema akitambulisha mkutano
Mwenyekiti wa CHADEMA, Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mh Freeman Mbowe akisisitiza jambo mkutanoni hapo jana (Picha zote na Jackson Wilson Mataka)
KWA PICHA ZA MATUKIO TOFAUTI ZAIDI UNAWEZA KUTEMBELEA BLOG ZA WANAHABARI EVARIST CHAHALI NA JOHN BUKUKU
0 maoni:
Post a Comment