Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mbunge mpya CHADEMA aahidi kutumia mshahara wake kusomesha watoto 100 Karatu

DSCN0188 Mbunge wa CHADEMA Viti Maalumu, Mh Cecilia Paresso aliechukua nafasi yamarehemu Regia Mtema aliefariki kwa ajali ya gari ametoa ahadi ya kugharamia watoto 100 waliokosa nafasi za kuendelea na masomo kutokana na umasikini wa wazazi wao mjini Karatu.

Cecilia aliyasema hayo katika mkutano mkubwa ulioandaliwa maalumu kwa mapokezi yake mjini Karatu anakotokea. Alisema atatumia mshahara wake wa kwanza kama shurkrani na kuwagharamia watoto hao ambao wamekosa fursa ya kupata elimu.

Katika mkutano huo uliovuta mamia ya wananchi, walikuwepo pia viongozi wengine wa CHADEMA kame Mh Godbless Lema na wanachama wengine wapya waliotambulishwa juzi akiwemo aliekuwa Diwani wa Sombetini, Alphonce Mawazo na aliekuwa Mwenyekiti Mahusiano UVCCM, Ndg Ally Bananga.

CHADEMA iliendelea kuvuna wanachama wapya ambapo zaidi ya wananchama 100 walijiengua CCM na kujiunga na chama hicho katika mkutano huo.

Source: Chanel Ten

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO