Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Majambazi wawapora wanachuo Arusha

MAJAMBAZI zaidi ya 20 wenye silaha za jadi na za moto wamevamia Chuo cha Uhasibu (TIA) kilichoko Njoro nje kidogo ya hapa na kupora vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 19.

Habari kutoka chuoni zilizothibitishwa na Polisi zilieleza kuwa uvamizi huo ulifanyika saa 8 usiku wa kuamkia juzi kwa majambazi hao kuingia chumba kimoja baada ya kingine na kupora vitu hivyo bila kudhuru mtu.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, mmoja wa wanachuo, Rajabu Lingoni alidai hawakuwa na jinsi ya kujinusuru kwani majambazi hao walikuwa wengi.

Lingoni alidai mbali ya kuwa na idadi hiyo, walikuwa na silaha za moto na za jadi yakiwamo mapanga, sime, mikuki na marungu na walisikika wakisema yeyote atakayepiga simu cha moto atakiona, hatua iliyofanya wanafunzi wakubali matokeo.

Alisema vitu walivyoporwa ni kompyuta 27, simu za mkononi aina mbalimbali zaidi ya 50 na viatu vya wanafunzi wote wa chuo hicho.
Mwanafunzi huyo alisema baada ya kufanya uhalifu huo, majambazi hao waliondoka na kuacha ‘mkwara mzito’, uliowafanya kutopiga simu Polisi usiku huo na hadi asubuhi walipowasiliana na Jeshi hilo kutoa taarifa.

“Hapa tulipo sasa tuko na Polisi na wanafanya uchunguzi wao, lakini wanafunzi wote wamesikitishwa na hali iliyojitokeza na kuwafanya kurudi nyuma sana kutokana na vitendea kazi vilivyoibwa, kwani tuliamrishwa kulala chini bila kupiga kelele na wao kuendelea kukusanya walichotaka,” alisema.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Thobias Andengenye alikiri kutokea uhalifu huo na kuahidi kutoa taarifa kamili jana.

Hata hivyo, hadi tunakwenda mitamboni, alikuwa hajaitoa. Kuvamia kwa kundi hilo la majambazi chuoni hapo, kunatia shaka kwani chuo kinalindwa na askari wa kampuni za ulinzi na haijulikani walikuwa wapi wakati majambazi hao wakiingia kufanya uhalifu huo.

Published by HabariLeo on 21st May 2012

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO