Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

NASSARI ATOA SADAKA YA SHUKURANI LEO

DSC00924 MBUNGE wa Arumeru Mashariki (CHADEMA), Mh Joshua Samwel Nassari (pichani kushoto) ametoa sadaka ya shukrani kwa Mungu kwa kumuwezesha kushinda katika majaribu yote kipindi cha uchaguzi wa Aprili 1, 2012 uliompatia Ubunge.

Nassari (26) alitoa sadaka yake hiyo katika Kanisa la Pentekoste Kilinga-Meru ambapo maelfu ya wananchi wa Arumeru na maeneo ya jirani walijumuika nae pamoja katika hafla kubwa iliyoandaliwa maalumu kwa ajili yake kutoa sadaka na neno la shukrani kwa waanchi waliomchagua.

Alipopewa nafasi ya kuzungumza, Nassari alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi wa Arumeru kuondoa tofauti zao na kuwakumbusha kuwa yeye ni Mbunge wa wananchi wote bila kujali dini, kabila wala itikadi ya mtu.

Alisema kuwa aliamua kutoa sadaka ya kumshukuru Mungu kwa mambo makuu aliyomtendea kabla ya kuanza ziara kwa wapiga kura wake, ambao wamekuwa wakimuita kwenye vijiji 86 vya jimbo hilo, kwani Mungu alimlinda kipindi chote, hata wakati wa kampeni magari yao matatu yalipata ajali kwa kuanguka, lakini hakuna aliyeumia huku yeye akiibuka na ushindi kwenye uchaguzi.

Akigusia swala la ardhi, Nassari alisema tatizo lililopo sio ardhi bali ni maono ya kuitumia ardhi hiyo. Aliwataka wananchi kabla ya kufikiria kupata ardhi, wahakikishe wamepata maono ya nini watakwenda kuifanyia ardhi hiyo.

Akitolea mfano Nassari alisema kuwa, yeye binafsi alikuwa na maono ya kuongoza toka akiwa mdogo, na kwamba alichofanya ni kupigana kuhakikisha anafikia ndoto hizo, licha ya hali ngumu ya kiuchumi kwenye familia yao, kiasi cha kumlazimisha akiwa na miaka 9 kuuza machungwa soko kuu la Arusha kila alipokuwa akitoka shule na mifuko ya plastiki kwenye soko la Tengeru na Mbauda.

Wageni mashuhuri waliohudhuria hafla hiyo iliyoanza majira ya saa 4 asubuhi hadi saa 11 jioni, huku watu wakila na kuwanya hadi kusaza, walikuwa ni pamoja na muasisi wa CHADEMA, Mzee Edwin Mtei, Mkuu wa zamani wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Jenerali Mirisho Sarakikya,na viongozi mbalimbali wa CHADEMA.

Wengineni Mbunge wa Iringa Mjini, Mh Mch. Peter Msigwa na Mbunge wa Mwibara, Mh Kange Lugora ambao wote walipata fursa ya kuzungumza na wananchi.

Mh Msigwa kwa upande wake, aliwataka watanzania kuliombea taifa Mungu alinusuru dhidi ya matukio maovu kama ambalo lilimkuta wiki iliyopita mjini Iringa na kunusirika kifo. Baadae wachungaji walimuwekea mkono na kumuombea.

Mchungaji  Msigwa  aliwataka viongozi wa dini kusimama kwenye ukweli daima na waepuke kutumiwa na wanasiasa wanaotaka kuyatumia vibaya makanisa kibiashara na kisiasa.

Lugora yeye alitumia muda mwingi kuelezea athari za rushwa na namna Serikali ya chama chake ilivyoshindwa kudhibiti vitendo vya rushwa nchini.

Alikmbushia zoezi la utiaji saini kukusanya kura za kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu na kueleza kuwa yupo katika wakati mgumu.

Alisema wakati wa fukuto la zoezi hilo, walikuwa wanatishwa na viongozi wa Serikali wasisaini fomu za Mh Zitto Kabwe na kuwaziba mdomo wasiseme, akadai kuwa yeye alikataa kuafikiana na vitisho hivyo na anamshukuru Mungu ameweza kuyasema yote.

Mbunge wa CCM adai kutishiwa maisha

MBUNGE wa Mwibara, Kungi Lugola (CCM), jana alieleza jinsi alivyotishiwa maisha yeye na wabunge wenzake, kutokana na hatua yao ya kukemea hadharani matumizi mabaya ya fedha za umma wakati wa kikao cha Bunge kilichopita, na kudai kama si ujasiri na maombi ya wachungaji wasingepata ujasiri huo.

Akizungumza katika ibada ya shukrani ya Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (CHADEMA) kwenye Kanisa la EPCT, Kilinga, iliyohudhuria na viongozi mbalimbali, akiwemo muasisi wa CHADEMA, Edwin Mtei na  alisema licha ya taifa kuwa na rasilimali nyingi, lakini wananchi wake ni masikini wa kutupwa kwa vile viongozi wengi wamepofushwa na rushwa na hawataki kuambiwa ukweli kuhusiana na ufisadi na rushwa wanayofanya.

Mbunge huyo alisema, tabia yake na baadhi ya wabunge wachache wa CCM walioamua kusema ukweli, ilikuwa mwiba kwa baadhi ya watendaji, na wengi wanaogopa kusema ukweli kwa kuhofia maisha yao, na kukiri kwamba ilibidi kwenye kikao cha Bunge kilichopita awaombe watumishi wa Mungu wamuombee apate ujasiri wa kuwasema wale waliokuwa wanadhulumu mali ya umma.

Kutokana na hali hiyo, Lugola aliwaomba viongozi wa dini kote nchini kuwaombea viongozi wa serikali ngazi mbalimbali, wakiwemo wabunge, mawaziri na rais ili kuwaepusha kupofushwa na rushwa na waweze kuwahudumia wananchi kwa uaminifu.

Akihubiri katika ibada hiyo, mchungaji kiongozi, Langael Kaaya alisema kuwa taifa linahitaji maombi ili kuwepo na mabadiliko ya kiuchumi katika nchi, na viongozi wafunguke kutoka kwenye vifungo vya rushwa.

Mchungaji huyo alikemea kwa nguvu juhudi zozote za kutaka taifa liruhusu ndoa za jinsia moja, ambapo alisema kuwa jambo hilo ni upumbavu, laana na chukizo kwa Mungu, hivyo akawataka waumini wote kuungana pamoja kulikemea.

Source: arusha255.blog na Grace Macha

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO