Wachimba migodi wa Zambia wamemuuwa meneja Mchina, kwa kumvurumishia kiberenge wakati wa ghasia.
Mchina mwengine alijeruhiwa na Wazambia kadha piya.
Wafanyakazi walikuwa wakilalamika juu ya pato, kwenye mgodi kilomita 325 kusini ya mji mkuu, Lusaka.
Walikereka kwa sababu mshahara wao ulikuwa kasoro ya kiwango cha chini kipya kilichowekwa na serikali, cha dola 220 kwa mwezi, kwa wafanyakazi wa madukani.
Waziri wa Madini wa Zambia amekwenda kwenye mgodi huo.
Mwaka wa 2010 , mameneja wawili wa Uchina walishtakiwa kwa jaribipo la mauaji, kwa kufyatua risasi mbele wa wachimba migodi waliokuwa wakiandamana.
Source: BBC
0 maoni:
Post a Comment