Published Wednesday, 08 August 2012
SIKU chache baada ya Serikali kuzitaka ndege zinazozunguka Ziwa Nyasa upande wa Tanzania kufanya utafiti wa mafuta kuondoka mara moja, Serikali ya Malawi imetii na kuziondoa kampuni zinazofanya kazi hiyo katika ziwa hilo.
Akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake Jumatatu iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe aliitaka Malawi kuziondoa ndege na kampuni zinazofanya utafiti wa mafuta katika eneo hilo kwa kuwa ni mali ya Tanzania.
Mbali na Waziri Membe, viongozi wengine waliozungumzia mgogoro huo na kuitaka Malawi iache uchokozi ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Edward Lowassa.
Wakati Sitta akiwataka Watanzania kuendelea na shughuli zao bila hofu kwa kuwa Serikali iko tayari kwa tishio lolote, Lowassa alisisitiza kuwa Tanzania imejiandaa kiakili na kivifaa kuingia vitani na Malawi kama italazimika kufanya hivyo
Click hapa kusoma habari yote kupitia Gazeti la Mwananchi
0 maoni:
Post a Comment