Tamasha la Simba Day limefanyika jana August 8, 2012 likiudhuriwa na wapenzi wengi wa mchezo wa mpila wa miguu. Klabu ya Simba ilikuwa ikionyesha uwezo wake kutokana na usajili waliofanya huku tukio hilo likienda sambamba na kuwaenzi wote waliofanikisha mafanikio ya Simba kwa namna moja hadi nyingine huku Mgeni wa Heshima Philemon Sarungi akitoa tuzo mbalimbali .
Tamasha lilishuhudia timu hiyo mabingwa watetezi wa ligi kuu wakipoteza mchezo wao wa kirafiki dhidi ya timu ya Nairobi City Star ya Kenya kwa goli 3 kwa 1. Simba walikuwa wa kwanza kupata bao kwa kupitia mchezaji wao tegemeo Felix Sunzu baada ya kuunganishiwa mpila kutoka kwa mchezaji mahiri Mwinyi Kazimoto mnamo dakika ya 15.
Timu ya Nairobi ilifanikiwa kusawazisha goli mnamo kipindi cha pili dakika ya 57 kupitia kwa Duncan Owiti,goli la pili la Nairobi City lilifungwa mnamo dakika ya 64 na mchezaji wao Bruno Okukku na huku la 3 likifungwa na Boniface Oyango mnamo dakika ya 79.
Awali ya mchezo huo ilitanguliwa na mechi ya timu za vijana wa kike kati ya Simba Queens dhidi ya Evergreen FC ya Temeke huku ikishuhudiwa Simba Queen wakiibuka na ushindi mnoo wa goli 5 kwa 3 ya Evergreen wafungaji wakiwa ni Maimuna Khamisi aliyefunga magoli 3,Rehema Kanta goli 1 na Grace Tony goli 1.
Kwa upande pinzani wa Evergreen FC wafungaji walikuwa ni Vumili Maarifa gioli 1,Shaida Boniface goli 1,Amina Sharabili goli 1
Uwanja wa Taifa kabla ya kuanza mpambano
Kikosi cha Simba SC kilichoxheza na Nairobi City Star ya Kenya jana
Kikosi cha Simba Queens kilichoumana na Evergreen ya Temeke, kwa timu za wananwake
Uhuru Selemani katika moja ya heka heka uwanjani katika mpambano wa kirafiki na Nairobi City Star jana
Simba Queens na Evergreen wakichuana vikali
Wachezaji wa Simba wakipasha misuli kabala ya kuanza mpambano wao hapo jana
Mrisho Ngassa akiweka viungo sawa
Magolikipa nao wakijifua vilivyo
Emmanuel Okwi akitabasamu na tuzo yake..
PICHA ZOTE NA MAELEZO: SPORTS EYE’S ALBUM ON FACEBOOK
0 maoni:
Post a Comment