*Lengo ni kudhibiti vitendo vya jinai
*Ikithibitika majina yao yatatumwa Beijing
*Kamati ya Makinda yasubiriwa kwa hamu
*Viongozi wa dini watishia kwenda majimboni
TUHUMA za rushwa zinazoendelea kuwaandama wabunge, zimechukua sura mpya, baada ya Serikali ya China kujiandaa kupiga marufuku wabunge wote wanaotuhumiwa kujihusisha na rushwa kuingia nchini humo.
Habari za uhakika ambazo (Gazeti) MTANZANIA imezipata kutoka ubalozi wa China hapa nchini, zinasema umepokea taarifa rasmi kutoka kwa viongozi wakuu wa China, wafuatilie kwa karibu wabunge wote wanaotuhumiwa kwa rushwa, kisha watume taarifa ili wakibainika wasiingie kwenye nchi hiyo.
“Tumeletewa taarifa na viongozi wetu wa ngazi za juu, kuwa tufuatilie kwa kina wabunge wote ambao wanatuhumiwa na wakibainika majina yao yatumwe China, ili wazuiliwe kuingia kule.
0 maoni:
Post a Comment